Skip to main content

Posts

MOROGORO: AKAMATWA AKIWA UCHI NA MTOTO MTONI

Mtu mmoja (Jina halijafahamika) anashikiliwa na Polisi baada ya kukutwa mtoni na mtoto mwenye umri kati ya miaka 5 na 10, wote wakiwa hawana nguo huku akiwa na panga na msumeno - Tukio hilo limetokea Desemba 19, 2019 katika Maporomoko ya Maji ya Nguzi Camp, na taarifa zinaeleza kuwa wakati mtu huyo akiwa katika Maporomoko hayo, Askari waliokuwa katika shughuli nyingine walimuona na kumtilia shaka - Inadaiwa kuwa, baada ya kuonekana alijitosa kwenye maji ya kina kirefu akiwa na mtoto huyo ambaye alikuwa akipiga kelele na kusema “baba unaniua, baba unaniua” - Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amesema atalitolea maelezo ya kina tukio hilo leo Jumamosi Desemba 21 katika mkutano na Waandishi wa Habari

MAREKANI YAPINGA ICC KUICHUNGUZA ISRAEL, ISRAEL YASEMA UCHUNGUZI HUO NI SILAHA YA KISIASA

- Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema nchi yake inapinga vikali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kufungua uchunguzi dhidi ya uhalifu unaotuhumiwa kufanywa na Israel - Pompeo amesema, hatua hiyo iliyotangazwa jana na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC inatafuta njia za kuielenga Israel katika namna isiyo ya Haki - Uamuzi huo wa ICC wa Madai ya Uhalifu wa Kivita katika eneo la Palestina umezusha majibu ya hasira kutoka Israel ambapo Wapalestina wameukaribisha uamuzi huo na kusema umechelewa kufuatia uchunguzi wa awali wa karibu miaka 5 tangu kuzuka kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza 2014 - Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameutaja uamuzi wa Mahakama hiyo ambayo Israeli ilikataa kujiunga nayo tangu ilipooundwa mwaka 2002, kuwa ni "Silaha ya Kisiasa" dhidi ya Taifa hilo la Kiyahudi - Hata hivyo, Netanyahu amesema Mahakama ya ICC haina uwezo wa kuchunguza yanayotokea ndani ya mipaka ya Palestina

Tetesi hizi ni mpya kuhusu pogba

 Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kwamba Paul Pogba "hatauzwa Januari" na pia amekanusha madai ya kwamba amekutana na mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland jana siku ya Ijumaa. Pogba, kiungo huyo wa kati wa United, amerejea baada ya kupata jeraha lakini pia amekuwa akihisi vizuri na kuna uwezekano mkubwa asicheze katika mechi dhidi ya Watford Jumapili ijayo. Wakati huo huo, kuna taarifa zinazodai kwamba Haaland amesafiri kutoka Stavanger Norway hadi Manchester na babake. Lakini Solskjaer amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ni "zawadi ya Krismasi". "Sidhani kama hatma yake ni hapa, amesema. "Siwezi kuzungumzia wachezaji wa timu nyengine. watu wataanza kuwa na mashaka na wewe." Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba alikuwa anatarajiwa kurejea katika kambi ya mazoezi wiki iliyopita baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguuni ambalo limemfanya kuwa nje tangu Septemba lakini akauguwa na hali yake ik

WhatsApp kuzimwa katika simu hizi mwaka 2020

WhatsApp kuacha kufanya kazi katika mamilioni ya simu kuanzia mwaka 2020. Simu hizi ni matoleo ya nyuma ya simu zinazotumia Android, iOS na Windows Phone. WhatsApp kuacha kufanya kazi: Je simu yako itaendelea kuwa na sifa? Kampuni ya WhatsApp inayomilikiwa na Facebook imetoa taarifa ikisema inasikitika na uamuzi huu ila ni uamuzi wa kilazima kufanyika ili kuhakikisha wanaendelea kuwa na uwezo wa kuhakikisha watumiaji wake wanakuwa salama dhidi ya udukuzi ambao unaweza kufanywa kwenye matoleo ya nyuma ya programu endeshaji za simu. Kwa watumiaji wa simu zenye sifa zifuatazo wajiandae kuona app ya WhatsApp ikisumbua kufanya kazi ifikapo Februari 1 2020, kama simu zao zinauwezo wa kupokea matoleo mapya ya programu endeshaji basi wanashauriwa kufanya hivyo. Simu za iPhone 5 na 5S kutoka Apple zinaonekana kuwa ni baadhi maarufu ambazo zitaathirika kwa uamuzi huu. Bado zinatumika hasa kwa mataifa yanayoendelea. Tovuti ya DeviceAtlas ilisema kufikia mwaka huu simu za iPhone 5 n

Simu Janja Mpya Kutoka Infinix: Jua Sifa Za Infinix S5!

Hivi unalikumbuka tolea la S4 kutoka simu za Infinix?  Naam! Ni moja kati ya yale matoleo yanayotoka katika  ‘S Series’ . Hivi Sasa kampuni ya Infinix inakuletea toleo lingine linalojulikana kama Infinix S5. Simu hii imekuja sambamba na msimu wa sikukuu hivyo tegemea promoseni ambayo ina zawadi kedekede kutoka kwao Infinix Ijulikane kwamba kwa sasa Infinix S5 ndio kinara wa matoleo ya ‘S Series’ kutoka Infinix, simu janja hii ina vipengele vya kuvutia kama vile ‘ Infinity-O Display’  na  Megapixel (MP) 32  katika kamera yake ya selfi . “Infinix ikiwa ni kampuni yenye ushawishi mkubwa katika mfumo wa kidigitali tunawahakikishia wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei Rafiki”- alisema afisa mahusiano Infinix, Aisha Kurupa Timu Ya Infinix Ikiwa Kazini SIFA ZAKE KWA UFUPI Kamera ya selfi ambayo ina MP 32 Kamera nne za nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens vile vile zikiwa na teknolojia ya Artificial Inteligency (AI) Memori ya uhifadhi wa ndani ni Gb 64 na

Google wameanza kusambaza teknolojia mpya ya SMS

Google wameanza kusambaza teknolojia mpya ya SMS yenye lengo la kuwa ndio teknolojia ya kuacha na ile iliyozoeleka kwa miaka mingi katika huduma ya ujumbe mfupi (sms). Katika kipindi cha zaidi ya mwaka na nusu kampuni ya Google imekuwa ikifanya mazungumzo na makampuni ya mitandao ya simu nchini Marekani juu ya uamuzi wake wa kutaka teknolojia mpya ya RCS iwe ndio teknolojia inayotumika kwa huduma za SMS. Ila imeonakana mitandao ya simu imekuwa kikwazo katika suala la kufanya maamuzi. Teknolojia ya SMS ya RCS ipoje? Teknolojia hii inawezesha app ya kawaida katika simu za Android kuweza kuwa na uwezo wa; Taarifa za ujumbe kuwa umesomwa au hapana Uwezo wa kujua kama mwingine anaandika muda huo Uwezo wa kuwa na makundi kwa urahisi (Groups) Google walikuwa na lengo la kuifanya teknolojia hii mpya ya SMS iwe ndio inayotumika kwa muda mrefu tuu. Katika mpango wao wa mwanzo walilenga kuhusisha mitandao ya simu katika utengekelezaji h Ila kutokana na hali ya kutopata ushirik

RUDI KWA MAMA

Wino huu uliomwagika umeandikwa Na yatima asiye Na baba wala mama! Mwenye machungu ya kumbukumbu kila atazamapo picha za wazazi wake! Mwenye tamaa yakuzungumza Na mama kumwambia anampenda! Nakushauriana na baba jinsi dunia inavyokwenda. Leo wino wangu umebeba dhamira yakukumbusha urudi kwa Mama. Usiseme hakuna sababu yamsingi yakwenda kumsalimia mama! Ukifanyacho kinakupa riziki, mafanikio na utajiri lakini vitu hivyo ni vichungu siku utakapokuwa huwaoni wazazi wako. Siku watakapokuwa mbali Na upeo wa macho yako! Siku nawewe utakapokuwa yatima. Rudi kwamama! Nenda kamwambie unampenda sana! Kaseme nae yote yakwako naumsikilize yote yakwake. Hakikisha anafarijika kwa uwepo wako! Usitoe hata dakika akahisi upweke! Akahisi umemtenga nakuzipa thamani kazi zako au watu wako wengine ulionao. Kumbuka wao wanakuona wamuhimu, mwenye nguvu Na wathamani! Kwasababu ya juhudi za wazazi wako. Walikesha nawewe ulipokuwa unawasumbua ukilia usiku kucha enzi za uchanga wako. Walihakikisha unanyamaza ha