Skip to main content

Posts

Showing posts with the label HIVI PUNDE

RIVER YAINYUKA ARSENAL

Jumamosi ya March 4 2017 katika Ligi Kuu  England  ilichezwa michezo kadhaa lakini usiku wake ndio ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu mchezo kati ya majogoo wa jiji la  Liverpool  dhidi ya  Arsenal The Gunners  wa  London . Arsenal  ambao leo wameripotiwa kumtafuta mbadala wa  Wenger  kutokea  Juventus , wamejikuta wakikutana na kipigo cha goli 3-1,  Liverpool  wamewafunga  Arsenal  wakiwa kwao na kufanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 52 na  Arsenal  wakifanya hivyo kwa silimia 48. Magoli ya  Liverpool  yamefungwa na  Roberto Firmino  dakika ya 9,  Sadio Mane  dakika ya 40 na  Georginio Wijnaldum  dakika ya 90, wakati goli pekee la  Arsenal  lilipatikana dakika ya 57 kupitia kwa  Danny Welbeck , matokeo hayo yanaifanya  Arsenal  kushuka hadi nafasi ya 5 wakiwa na point 50, huku  Liverpool  wakipanda hadi nafasi ya tatu kwa point 52. Msimamo wa Ligi Kuu England ulivyo kwa sasa baada ya kuchezwa mechi za March 4 2017.