Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Siasa

MOROGORO: AKAMATWA AKIWA UCHI NA MTOTO MTONI

Mtu mmoja (Jina halijafahamika) anashikiliwa na Polisi baada ya kukutwa mtoni na mtoto mwenye umri kati ya miaka 5 na 10, wote wakiwa hawana nguo huku akiwa na panga na msumeno - Tukio hilo limetokea Desemba 19, 2019 katika Maporomoko ya Maji ya Nguzi Camp, na taarifa zinaeleza kuwa wakati mtu huyo akiwa katika Maporomoko hayo, Askari waliokuwa katika shughuli nyingine walimuona na kumtilia shaka - Inadaiwa kuwa, baada ya kuonekana alijitosa kwenye maji ya kina kirefu akiwa na mtoto huyo ambaye alikuwa akipiga kelele na kusema “baba unaniua, baba unaniua” - Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amesema atalitolea maelezo ya kina tukio hilo leo Jumamosi Desemba 21 katika mkutano na Waandishi wa Habari

MAREKANI YAPINGA ICC KUICHUNGUZA ISRAEL, ISRAEL YASEMA UCHUNGUZI HUO NI SILAHA YA KISIASA

- Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema nchi yake inapinga vikali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kufungua uchunguzi dhidi ya uhalifu unaotuhumiwa kufanywa na Israel - Pompeo amesema, hatua hiyo iliyotangazwa jana na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC inatafuta njia za kuielenga Israel katika namna isiyo ya Haki - Uamuzi huo wa ICC wa Madai ya Uhalifu wa Kivita katika eneo la Palestina umezusha majibu ya hasira kutoka Israel ambapo Wapalestina wameukaribisha uamuzi huo na kusema umechelewa kufuatia uchunguzi wa awali wa karibu miaka 5 tangu kuzuka kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza 2014 - Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameutaja uamuzi wa Mahakama hiyo ambayo Israeli ilikataa kujiunga nayo tangu ilipooundwa mwaka 2002, kuwa ni "Silaha ya Kisiasa" dhidi ya Taifa hilo la Kiyahudi - Hata hivyo, Netanyahu amesema Mahakama ya ICC haina uwezo wa kuchunguza yanayotokea ndani ya mipaka ya Palestina

yajue mambo 5 ya mafanikio kwako

Kila binadamu ameumbwa na kiu ya kufanikiwa katika kila kitu anachofanya. Mafanikio ndio kilele cha mlima mkubwa wa maisha ambao umejengwa kwa misingi na ngazi za mihangaiko na mitihani ambayo unapaswa kuivuka ili upumzike kwenye kilele hicho. Kwa bahati mbaya, unaposema ‘mafanikio’ wengi hufikiria kuhusu ‘utajiri’. Lakini ukweli ni kuwa kuna tofauti kati ya kuwa tajiri na kufanikiwa kiuchumi. Unaweza kuwa tajiri lakini ukawa bado hujafanikiwa. Kwa kuwa watu wanawaza utajiri kuwa ndio kigezo cha mafanikio hujikuta wakijiingiza kwenye vitendo vya ajabu kwa lengo la kujizolea mali lakini mwisho huwa wanagundua kuwa hawajafanikiwa japo jamii inahisi wamefanikiwa. Njia rahisi za Kumgeuza Rafiki kuwa ‘Mpenzi Wako’ wa Dhati Nanachoamini mimi, kufanikiwa kweli ni kutimiza malengo yako kwa ufanisi na kwa wakati, lakini mafanikio hayo yakupe amani moyoni mwako (peace of mind). Vinginevyo, utafanikiwa kwa mrundikano wa fedha huku ukitengeneza tatizo kubwa zaidi la msongo wa mawazo na u

zinduka,, hizi ni njia za mafanikio

MTU anafanikiwa kikweli kwa kupata njia bora kabisa ya maisha ambayo inatokana na kufuata viwango vya Mungu na kuishi kupatana na kusudi la Mungu kwa wanadamu. Biblia inasema kwamba mtu anayeishi maisha ya aina hiyo “atakuwa kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao hutoa matunda yake katika majira yake na ambao majani yake hayanyauki, na  kila jambo analofanya litafanikiwa.” — Zaburi 1:3 . Naam, ingawa sisi si wakamilifu na tunafanya makosa, tunaweza kufanikiwa maishani! Je, hilo linakuvutia? Ikiwa ndivyo, basi kanuni sita zinazofuata za Biblia zinaweza kukusaidia ufikie lengo hilo na hivyo kuthibitisha waziwazi kwamba kwa kweli mafundisho ya Biblia ni hekima inayotoka kwa Mungu.— Yakobo 3:17 . 1 Uwe na Maoni Yanayofaa Kuhusu Pesa “Kupenda pesa ni chanzo cha mambo mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo wengine . . . wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi.” ( 1 Timotheo 6:10 ) Ona kwamba tatizo si pesa, kwa kuwa sisi sote tunahitaji pesa

TRA kumchunguza Askofu Kakobe baada ya kumsikia akisema ana hela kuliko Serikali

 Kufuatia Kauli ya Askofu Kakobe kusema "Nina hela kuliko Serikali" sasa TRA wapanga kumchunguza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema; Watu wa Kodi (TRA) wanasema wamepokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao TRA wanaendelea na kusema; Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema Hivyo Askofu Kakobe ni tajiri sana kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania TRA wanasema wanawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe wakaanza kupitia kumbuk

MUGABE APEWA SIKU KUACHIA MADARAKA, VIONGOZI WAJIPANGA KUMFUNGULIA MASHTAKA YA UHALIFU

Waziri wa chama c cha Zanu-PF cha Zimbabwe wanajitayarisha kukutana na kujadili uhalifu wa Rais Robert Mugabe, baada ya mwisho wa kujiuzulu kwake na kuja Jumatatu. Siku ya mwisho iliwekwa na chama cha Mugabe mwenyewe, Zanu-PF. Kiongozi huyo alisisitiza wananchi wa Zimbabwe siku ya Jumapili, akitangaza kwenye TV kwamba alipanga kubaki kama rais. Zanu-PF inasema kuwa ni nyuma ya uhalifu, na kesi zinaweza kuanza mapema Jumanne wakati bunge litakutana. Ushiki wa Mugabe juu ya nguvu umepungua sana tangu jeshi la nchi liliingilia Jumatano mfululizo juu ya nani atakayefanikiwa. Mgogoro huu ulianza wiki mbili zilizopita wakati kiongozi mwenye umri wa miaka 93 alipomfuta kazi naibu wake Emmerson Mnangagwa, makamanda wa jeshi  waliiona kama ni jaribio la kumuweka mke wake Grace kama Rais wa pili. Zimbabwe tangu wakati huo imekua na mikutano mikubwa ya barabara inayoshinikiza  kujiuzulu kwa Mugabe mara moja. Maandamano hayo yamesaidiwa na wapiganaji wa Vita walioathiriwa - ambao walipi

WACHINA WATIWA MBALONI DAR ES SALAAM

Raia wanne wa China wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuendesha kiwanda cha kutengeneza mifuko ikiwemo ya plastiki kinyume na sheria huku kiwanda hicho kikitozwa faina ya shilingi Milioni 7 kwa makosa ya kisheria. Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakati wa ziara yake jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa raia hao wa kigeni wamekiuka taratibu na sheria za uendeshaji kiwanda kilichopo kwenye makazi ya watu na kuagiza kifungwe kwa muda ili kupisha uchunguzi wa usajili wake. Amesema serikali inawapenda wawekezaji kwenye sekta ya viwanda na inataka waje kwa wingi kuwekeza nchini lakini ni lazima nao wafuate sheria za nchi katika uwekezaji wao ili kila upande uweze kufaidika na uwekezaji huo.

DKT LOUS SHIKA TAYARI KUTUMIWA MABILION YAKE KUTOKA URUSI

Dkt. Louis Shika ambaye alijizolea umaarufu baada ya kutangaza dau kununua nyumba tatu za mfanyabiashara Said Lugumi kwa shilingi bilioni 3.2 zilizokuwa zikipigwa mnada na kampuni ya Yono lakini akashindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo, ameanza mchakato wa kurejesha fedha zake zilizopo nje ya nchi. Amesema kuwa leo jumamosi amelipa Dola 100 za Kimarekani sawa na shilingi (220,000) za Kitanzania kwa ajili ya bima ili aweze kutumiwa fedha zake nchini. Dkt. Shika amesema hayo mara baada ya kukutana na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alipokuwa ametembelea Shirika la Posta kuzungumza na wafanyakazi, walimkuta Dkt. Shika akiwa katika shirika hilo, na kudai kuwa yupo hapo kwa ajili ya malipo. “Nimelipa dola 100 za bima ili kukamilisha fedha zangu zije na nilipie zile nyumba, hili la bima lilikuwa ni muhimu sana kwangu,”amesema Dkt. Shika Hata hivyo, nyumba moja ilishauzwa kwa mhindi aliyeshika namba mbili

MAUAJI DAR: Maiti tatu zadaiwa kuokotwa ufukweni Coco Beach

  ​ Maiti za wanaume watatu zimekutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo kati ya hizo moja imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba. Wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo wamesema juzi wakiwa kwenye biashara zao asubuhi ghafla waliona maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikifungwa na kamba. Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi na kuichukua kwenye gari lao. Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alitoa taarifa polisi baadaye zilichukuliwa. "Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona jana ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake," amesema Ally. Mfanyabiashara mwingine Issa Isaya amesema cha kushangaza maiti zinazo

Mwigulu Nchemba: Aliyemtisha Nape kwa bastola sio Polisi. Uchunguzi wa Lissu kushambuliwa unaendelea, tutatoa taarifa

Waziri wa mambo ya ndani atafanya mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 na watangazaji wanadhamiria kumuuliza juu ya matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana. Wale mlio majumban mkiangalia mtupe updates sisi tusio karibu na luninga. Asubuhi njema. Tutegemee siasa chafu hapo =============================================== KUHUSU MAUAJI YA KIBITI => Natoa pole kwa familia zote zilizopoteza watu wake. => Jukumu la kwanza kubwa la serikali ni usalama wa kila raia na ikitokea kushambuliwa au kuuliwa kwa mtanzania yoyote hilo ni pigo kwetu. => Kama wizara haki ya kwanza tunayoilinda ni usalama wa kila mtanzania. => Hatutaruhusu uhalifu utawale eneo lolote lile la nchi yetu na swala la kukabiliana na uhalifu halina ukomo. => Hata pale panapokuwa salama bado tutaendelea kulinda na sio kubweteka. => Hatukuchelewa kwenda kibiti mauaji yalipoanza ila ni kutokana na muundo wetu wa vyombo vya usalama. Tulikuwepo kibiti na ni suala la muda tuu. => Swala la mapambano na