Waziri wa mambo ya ndani atafanya mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 na watangazaji wanadhamiria kumuuliza juu ya matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana. Wale mlio majumban mkiangalia mtupe updates sisi tusio karibu na luninga. Asubuhi njema. Tutegemee siasa chafu hapo
===============================================
KUHUSU MAUAJI YA KIBITI
=> Natoa pole kwa familia zote zilizopoteza watu wake.
=> Jukumu la kwanza kubwa la serikali ni usalama wa kila raia na ikitokea kushambuliwa au kuuliwa kwa mtanzania yoyote hilo ni pigo kwetu.
=> Kama wizara haki ya kwanza tunayoilinda ni usalama wa kila mtanzania.
=> Hatutaruhusu uhalifu utawale eneo lolote lile la nchi yetu na swala la kukabiliana na uhalifu halina ukomo.
=> Hata pale panapokuwa salama bado tutaendelea kulinda na sio kubweteka.
=> Hatukuchelewa kwenda kibiti mauaji yalipoanza ila ni kutokana na muundo wetu wa vyombo vya usalama. Tulikuwepo kibiti na ni suala la muda tuu.
=> Swala la mapambano na uhalifu ni endelevu na hali ilivyokuwa mwanzo na sasa ni tofauti na bado tunaendelea na usalama.
=> Tunawahakikishia watanzania kwamba tutapambana na wahalifu wa aina zote.
=> Tulichokifanya ili kupambana na uhalifu huu ni kuongeza vitendea kazi, tumeufanya kuwa mkoa wa kipolisi na tunaendelea kutafuta taarifa zinazohusu uhalifu ili kuuthibiti kabla haujatokea.
KUHUSU MIILI KUOKOTWA BAHARINI
=> Waliokufa Tanga bado tukio hilo linaendelea kufanyiwa kazi na tumeelekeza uchunguzi wa kina ufanyike na baada ya hapo tutatoa taarifa ya nini kilitokea. Kitu pekee ambacho kinachunguzwa ni chanzo cha tukio zima kutokea.
=> Uchunguzi kuhusu miili inayotupwa tumegundua kwamba kuna watu wasio wema ambao wamekuwa wakifanya biashara haramu ya binadamu na kuwabeba watu hao kama bidhaa na kuwajaza kwenye fuso.
=> Hii inasababisha wakose hewa ya kutosha hivyo wakifariki wanawatupa.
=> Mara nyingi wanawatupa majini. Na wengine 80 walitupwa mpakani mwa Tanga na Bagamoyo na walikuwa mahututi sana hawawezi hata kuongea.
=> Hivyo sababu mojawapo ya miili inayookotwa ni biashara haramu ya binadamu.
=> Hivyo tunafanyia kazi matukio haya ili kuwatambua wahusika wa matukio haya.
KUHUSU KUSHAMBULIWA KWA LISU
=> Kuna vitu vingi ambavyo bado tunasita kuvisema hadharani lakini wananchi wawe na imani na kazi ambayo tunaendelea kuifanya na watapewa taarifa.
=> Uchunguzi ulianzia eneo la tukio aliposhambuliwa na kuna taarifa zimeshachukuliwa kutoka maeneo mbalimbali ambazo zinahusiana na tukio hili na zinafanyiwa kazi.
=> Ni tukio linaloudhi na tunahakikisha kwamba tunapata undani wake na kuwapata wanaohusika.
=> Hakuna ukomo wa uchunguzi mpaka pale uchunguzi utakapokamilika na matukio haya ya watu kushambuliwa yameshakuwa mengi tofauti na hili la Lisu.
=> Sio matukio yote yanayohusisha polisi kushambuliwa ndio watuhumiwa hupatikana haraka bali ni utofauti wa mazingira na vifaa vinavyotumika ndivyo vinarahisisha au kukwamisha kwa watuhumiwa kukamatwa kwa haraka.
=> Hatubagui watu kwa itikadi zao wala rangi zao bali ni kila mtanzania bali ni mazingira ya tukio ndiyo yanahusika sana kwenye uchunguzi.
=> Tumeshakamata magari zaidi ya 10 ambayo yanafanana na gari lililofanya tukio. Hatuwezi kusema zaidi kwasababu ni mambo ya ndani sana ya kiuchunguzi na siwezi kuyasema hadharani kutokana na jambo lenyewe kuwa ni nyeti sana mpaka litakapokuwa tayari.
=> Serikali tunaendelea kupata taarifa za maendeleo ya afya yake kupitia balozi lakini mimi binafsi sijaenda.
=> Kwa taratibu zetu kuna watu ambao wanafanya kazi ya kuwasiliana naye pamoja na dereva wake ili kuweza kupata taarifa zinazoweza kusaidia kwenye uchunguzi.
=> Sisi tunatamani sana dereva asaidie kwenye kutoa taarifa sababu tunazani angeweza kutusaidia taarifa nyingi hata magari tuliyakamata tulitegemea yeye atusaidie kuja kuyatambua maana yeye aliliona gari husika.
=> Ila alipoitwa na polisi Dodoma watanzania wengi walilichukuliwa swala hili kwa mtazamo hasi na kudhani kwamba polisi wanataka kumkamata dereva lakini hapana, Nia yetu ni kutaka kushirikiana naye kwenye uchunguzi wa tukio hili.
KULETA WATU KUTOKA NCHI ZA NJE KUFANYA UCHUNGUZI
=> Tunashughulika na usalama wa raia wetu pamoja na matukio yanayowadhuru raia wetu.
=> Kazi inayofanywa na jeshi la polisi ni kubwa sana ila tu kwasababu hatuwezi kusema hadharani jinsi kazi inavyofanywa ndio maana wengi hawajui.
=> Sisi kama wizara hatutapenda kuitangazia nchi kwamba jambo la usalama wa nchi na raia kwamba limetushinda. Hii itakuwa jambo la aibu sana kwa nchi hata dunia nzima.
=> Tunataka kila shambulio la umwagaji damu ya mtu yoyote uchunguzi wake uwe mkubwa zaidi kuliko matukio mengine tunayoyafanya kikawaida.
=> Kila kifo kikishatokea au shambulio la kutaka kuua mtu inatakiwa uchunguzi ufanyike wa kina.
=> Mfano kifo cha Mtikila kilijadiliwa sana hivyo halitakiwi kuchukuliwa kama jambo la kawaida, Pia kupotea kwa Ben saanane.
=> Watu wengi ni waoga wa kutoa taarifa za matukio mabaya yanayotokea na hii inaleta ugumu kwenye taasisi yangu kulishughulikia hili.
NAPE KUONYWESHWA BASTOLA HADHARANI
=> Hili tumeshalisema sana
=> Kuna vitu vilionekana kuwa dhahiri lakini baada ya uchunguzi haikuwa hivyo.
=> Tulidhani kijana yule ni polisi lakini baada ya uchunguzi tulibaini kwamba hakuwa polisi. Na kijana yule hakuwa na sare.
=> Hivyo kwakuwa hakuna sare muhalifu pia alikuwa na nafasi ya kutumia nafasi hiyo kufanya uhalifu wake na kwa kuwa hakuwa na sare inakuwa ngumu kumtambua.
=> Suala la ulinzi kwa viongozi yapo kwa mujibu wa sheria lakini kuna baadhi ya wabunge sheria haijawasemea kwamba wawe na walinzi hivyo tunashughulikia hili kwa sasa.
=> Tutaongeza ulinzi kwenye maeneo yote ya viongozi na kufanya doria za mara kwa mara.
=> Baada ya Lisu kusema anatishiwa maisha tuliongeza ulinzi lakini shida ni jinsi alivyokuwa anatoa taarifa hadharani hii ingeweza hata kuwapa mwanya wale waliokuwa wanapanga njama za kumdhuru kujipanga zaidi.
=> Alipotaja gari inayomfwatilia niliagiza gari hiyo itafutwe na suala hilo lilifanyika na watu waliopatikana walihojia lakini gari ikaonekana kuwa tofauti na ile aliyoitaja na gari hiyo ilionekana kwamba haijafanya safari yoyote kwenye maeneo ambayo Mhe Lisu alikuwepo.

Post a Comment