Skip to main content

MAHAKAMANI: VIGOGO WALIOKWEPA KODI NA KUSABABISHA HASARA YA BILIONI 29

Upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia hasara ya Tsh Bilioni 29 Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ inayowakabili watu watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka hiyo, Reuben Mwakasa, bado haujakamilika.

Mbali na Mwakasa, mkazi wa Msagara, Moshi, Kilimanjaro, washitakiwa wengine ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, mkazi wa Makongo Juu.
Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika ambapo, baada ya kueleza hayo Hakimu Mwijage ameahirisha kesi hiyo hadi October 11, 2017.
Washtakiwa hao wanadaiwa walitenda kosa hilo, kati ya November 22, 2013 na August 21, 2017, katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Temeke na Ilala.
Inadaiwa washitakiwa hao kwa pamoja vitendo vyao waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho kwa kukwepa kulipa kodi.

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD; nyimbo mpya ya alikiba #JOHOTENA

Jinsi ya ku-track simu yako na kujua mahali ilipo

Upotevu wa simu yako ni moja ya jambo baya watu wanalipata.Unaweza kuibiwa simu yako iliyokuwa imehifadhi data nyingi binafsi. Kwa msaada jinsi ya kupata simu yako iliyopotea, Google na Apple kwa pamoja wana njia za kufuatilia hili kutafuta mfumo wa simu yako. Jinsi ya kutafuta iPhone iliyopotea Ufumbuzi wake upo kwenye Find My iPhone.Huduma hii ina uwezo wa kukuonyesha kifaa chako chochote cha iOS Kupata uwezo juu ya iPhone yako,fuata hatua hizi; 1.Nenda kwenye setting/mpangilio wa iPhone yako 2.Shuka chini utakuta iCloud 3.Katika chini ya orodha bonyeza "Find My iPhone" 4.Kwenye Find My Phone switch on position 5.Ukiwa hapo ni wazo zuri ku-turn on send last  location Baada ya kuwezesha Find My iPhone,unaweza kuifuatilia vizuri simu yako iliyopotea na kuibiwa Jinsi ya kupata Android phone Kwa android ni tofauti kidogo na Apple.Google wameweka app yao kwenye Play store  na unaweza ku-download 1.Search Play Store "Android Device Manager" 2.Inst

Tumia simu yako kama mounse ya komputa

New Trick Habari za wakati huu msomaji wa Blog yako pendwa ya  DODY BLOG ! Katika mfululizo wa makala za wiki hii, leo tutaangalia jinsi ya  KUTUMIA   simu yako hio ya  SmartPhone kama  Mouse  ya kompyuta. FAIDA >>>Hii inaweza kukusaidia pale ambapo hauna Mouse kwa ajili ya compyuta yako, au  TouchPad  ya Laptop yako haifanyi kazi! Yani  inasumbua! MAHITAJI >> Utahitajika kuinstall program na App ntakazokupa hapa chini! Unaweza kutumia Apps mbalimbali na step ni hizihizi.  Host file utaiinstall kwenye kompyuta yako na App utaiweka kwenye simu yako, halafu utaunga compyuta yako kwenye wireless ya simu yako au bluetooth!  (Lengo la kuunga ni kuweka mawasiliano kati ya simu na kompyuta). kwa hio unaweza kutumia  Bluetooth au Wireless!  Zote ni sawa ila hapa nitaelezea Wireless. HATUA KWA HATUA 1.   Download na install  Monect  kwenye simu yako  HAPA! Install Monect Portable 2. Kwenye PC yako download na install  Monect Host  kwa kuclik  HAPA