Wino huu uliomwagika umeandikwa Na yatima asiye Na baba wala mama! Mwenye machungu ya kumbukumbu kila atazamapo picha za wazazi wake! Mwenye tamaa yakuzungumza Na mama kumwambia anampenda! Nakushauriana na baba jinsi dunia inavyokwenda. Leo wino wangu umebeba dhamira yakukumbusha urudi kwa Mama. Usiseme hakuna sababu yamsingi yakwenda kumsalimia mama! Ukifanyacho kinakupa riziki, mafanikio na utajiri lakini vitu hivyo ni vichungu siku utakapokuwa huwaoni wazazi wako. Siku watakapokuwa mbali Na upeo wa macho yako! Siku nawewe utakapokuwa yatima. Rudi kwamama! Nenda kamwambie unampenda sana! Kaseme nae yote yakwako naumsikilize yote yakwake. Hakikisha anafarijika kwa uwepo wako! Usitoe hata dakika akahisi upweke! Akahisi umemtenga nakuzipa thamani kazi zako au watu wako wengine ulionao. Kumbuka wao wanakuona wamuhimu, mwenye nguvu Na wathamani! Kwasababu ya juhudi za wazazi wako. Walikesha nawewe ulipokuwa unawasumbua ukilia usiku kucha enzi za uchanga wako. Walihakikisha unanyamaza ha