SIMULIZI YA KOSA LANGU:

SIMULIZI YA KOSA LANGU: 
AUTHOR : ADELA DALLY KAVISHE
Joyce ni msichana aliyezaliwa katika familia ya watoto wawili akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mzee Ndesanjo, maisha yao yalikuwa ni maisha ya furaha na amani walikuwa wakiishi Mkoa wa Dar es salaam maeneo ya Kimara Stop Over, lakini furaha hiyo ilipotea baada ya siku moja ambapo Mzee Ndesanjo alikuja nyumbani baada ya kutoka kazini na moja kwa moja akimtaka mama Joyce ajiandae kwani wangesafiri siku hiyo ambapo ilikuwa ni siku ya jumanne mida ya saa kumi na mbili jioni.Mzee Ndesanjo alikuwa na gari aina Eskudo alifika na kuita kwa sauti "Mama Joyce Mama Joyce" huko chumbani mama Joyce alimskia na kuitika "Bee Mume wangu,vipi mbona unaonge kwa sauti sana si ungeingia ndani kwanza" alisema mamaJocye huku akiwa anamuangalia mume wake kwa makini Baba Joyce alimsogelea huku akisema "hakuna muda wa kupoteza mimi ndani siingii nenda kajiandae tunasafari ya kwenda Morogoro kuna matatizo kwani rafiki yangu tunayefanya naye kazi  amefiwa na mke wake wake inabidi tuwahi kwenda"

mama Joyce alinyamaza kimya kidogo kana kwamba kuna kitu anatafakari na kusema "mmmh jamani ni nini tena kilimfika kwani alikuwa anaumwa masikini" aliongea kwa masikitiko Baba Joyce akamjibu na kusema "alikuwa anaumwa na ameugua kwa muda mfupi sana,wewe nenda kajiandae tuondoke"  mama Joyce akasema "Lakini mume wangu watoto tutawaacha na nani" aliuliza mama Joyce kwani kwa wakati huo Jocye na mdogo wake aliyeitwa James walikuwa wameenda shule Joyce alikuwa darasa la tano na James akiwa darasa la kwanza na pale walipokuwa wakiishi likuwa ni nyumba ya kupanga.Baba Joyce alimgeukia tena mke wake na kusema "hawa watoto tutamkabidhi jirani yetu Mzee Ngonyani na mkewe kwani hatuendi kukaa zaidi ya siku mbili wewe jiandae tuondoke wakirudi kutoka shule watakuta maagizo kutoka kwa mke wa Ngonyani" alisema baba Joyce.

Ndipo mama Joyce akaenda kwenye chumba cha Mke wa Ngonyani na kumwachia maagizo ya kuwaangalia watoto wake kwa kipindi cha siku mbili baada ya hapo aliingia chumbani na kujiandaa tayari kwa safari ambapo safari ilianza wakiwa njiani maeneo ya  Kidatu ghafla gari lilipata pancha tairi ya mbele na kupinduka ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani Baba Joyce alifariki palepale na Mama Jocye alikuwa ameumia sana sehemu za kichwani hivyo wasamaria wema walimchukua na kumkimbisa hospitali,,,,nini kilitokea itaendelea

KOSA LANGU SEHEMU YA PILI

Baada ya wasamaria kumkimbiza hospitalini Mama Joyce ambaye kwa wakati huo alikuwa hajitambui  Askari  Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu wa Baba Joyce na kuupeleka chumba cha maiti hospitali ya Morogoro, gari lilikuwa limeharibika sana kutokana na ajali ilivyokuwa mbaya hivyo ulifanyka utaratibu wa kulisogeza hadi kituo cha polisi, wakiwa hospitalini Mama Joyce alikuwa hajitambui kabisa na hivyo Polisi waliamua kufanya utaratibu wa kufahamu ndugu ambao wangeweza kuwa naye karibu kwa wakati huo, mmoja wa mapolisi alimwambia mwenzake "sasa tutafanyaje kuwapata ndugu wa hawa watu kwani huyu mama hajitambui na mume wake amekwisha fariki inabidi tuwatafute ili waendelee na taratibu nyingine" mwenzake ambaye alikuwa naye akamjibu na kusema  "inabidi tupekue namba za simu katika simu zao na kuweza kuwasilia na ndugu zao" basi moja kwa moja alichukua simu ambayo ilikuwa ni ya baba Joyce na kuangalia namba za watu mbalimbali akiwa anatizama nani wa kumpigiia simu alijaribu jina ambalo lilikuwa kwenye simu ambalo liliandikwa Mkurugenzi alipiga namba hiyo bila mafanikio na alijaribu namba kama tatu zote zilikuwa hazipatikani.
Image result for kosa languRelated image
Ndipo wakaamua kuchukua simu ya mama Joyce na kuangalia namba nyingine katika simu hiyo kwa bahati nzuri walikuta namba ya Mke wa Ngonyani ambayo ilikuwa imeandikwa Mama ngonyani na kujaribu kuipiga simu iliita kwa mara ya kwanza bila kupokelewa hadi ikakata lakini waliendelea kujaribu hatimaye simu ilipokelewa,Mama Ngonyani ambaye ni jirani wa Mama Joyce aliyekuwa amekabidhiwa watoto alipokea ile simu akijua mke wa Ndesanjo ndiye aliyempigia na kusema "Habari mama joyce nilikuwa mbali na simu vipi mmekwishafika" yule askari aliyekuwa anasikiliza ile simu alinyamaza kimya kidogo na kusema "samahani mama unazungumza na askari polisi kutoka Morogoro" kabla hajaendelea Mama Ngonyani alimkatisha na kusema kwa mshangao "askari! kwani kuna nini tena mama Joyce yuko wapi?" aliuliza mama Ngonyani yule askari akamwambia usijali mama nilikuwa nataka kufahamu unamfahamu vipi Mama Joyce" kwa haraka Mama Ngonyani akajibu "Mama Joyce ni jirani yangu na pia ni rafiki yangu na wameenda Morogoro kwenye msiba sasa nashangaa kuzungumza na askari kupitia simu yake kwani kuna tatizo" alizungumza mama Ngonyani huku akitaka kufahamu nini kinaendelea ndipo yule askari akamwambia kile kilichotokea "Mama Joyce na mume wake wamepata ajali  maeneo ya kidatu na hapa ninapozungumza nipo hospitali ya Morogoro nilikuwa naomba ungewajulisha ndugu zake ili waje haraka" alizungumza yule askari lakini hakumwambia kama baba Joyce alikuwa amefariki.

kwa mshtuko mama Ngonyani akasema "Ajali? Mungu wangu jamani, kwahiyo wanaendeleaje sasa ndugu zake akinanani mimi ninachojua hawana ndugu zaidi ya watoto wao wawili Joyce na James ambao wapo hapa nyumbani na ni watoto wadogo sijui nifanyeje jamani" alizungumza maneno mengi kana kwamba mtu aliyechanganyikiwa kumbe masikini Mzee Ndesanjo na mke wake walikuwa hawana ndugu zaidi ya watoto wao yule askari alimsisitiza mama Joyce afike hospitali kwani kulikuwa hakuna mtu wa kumuhudumia mama Joyce basi Mama Ngonyani alimjulisha mumewe na haraka walijiandaa kwa safari ya Morogoro huku wakiwaacha Joyce na James bila kuwajulisha kile kilichotokea walipofika haospitalini ndipo walipogundua kuwa Baba Joyce alikuwa amefariki na hali ya mama Joyce ilikuwa mbaya sana walionana na daktari ambaye aliwaeleza iwapo mama Joyce akizinduka kuna uwezekano asikumbuke chochote kilichotokea kwani alikuwa ameumia sana maeneo ya kichwani maneno hayo yaliwasikitisha sana Mama Ngonyani na mume wake ambao waliamua kufanya utaratibu wa mazishi wakati huo Mama Joyce akiwa hajitambui walimuhamishia hospitali ya Muhimbili Dar es salaam  kuendelea na matibabu na huko nyumbani mazishi yalifanyika vilio na simanzi vilitawala watoto walilia sana kwa uchungu wakati huo na hata kupoteza fahamu huku wakiwa hawajui ni hatma ya mama yao mzazi hapo ndipo maisha ya Joyce na mdogo wake  yalianza kubadilika nini kitaendelea usikose sehemu ya tatu............

SIMULIZI YA KOSA LANGU SEHEMU YA TATU

Baada ya kumuhifadhi Marehemu kwenye makazi yake ya milele, watu walitawanyika pale nyumbani na kuwaacha akina Joyce wakiwa na simanzi na wakati huo waliishi kwa kumtegemea Mzee Ngonyani na mke wake,maisha yaliendelea huku baadhi ya watu wakitoa michango yao kwa ajili ya matibabu ya Mama Joyce ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Yule rafiki yake na marehemu mzee Ndesanjo alirudi Dar es salaam baada ya mazishi ya mke wake kule Morogoro na muda wote alikuwa hajui nini kimempata rafiki yake kipenzi kwani hata marafiki zake walimficha kwasababu naye pia alikuwa katika matatizo ya kufiwa na mke wake, aliporudi Dar es salaam alielekea nyumbani kwa marehemu ili kumjulia hali alipofika alimkuta Mama Ngonyani akiwa pamoja na Joyce wakiwa wanajiandaa kwenda hospitali kumuona mgonjwa Joyce alikuwa akimfahamu rafiki wa baba yake ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Beni basi alipomuona akaanza kumfuata huku akilia kwa uchungu “Baba mdogo Baba mdogo, ulikuwa wapi Baba yangu amefariki na mama anaumwa sana” Mzee Beni alimuangalia Joyce kwa makini kisha akasema “etii!Mzee Ndesanjo amefariki haiwezekani jamani nini kilitokea,siamini mimi haya maneno” alizungumza huku akiwa amemshika mkono Joyce aliyekuwa analia kwa uchungu.



Mama Ngonyani akamsimulia kila kitu kuhusu ajali waliyoipata marehemu Mzee Ndesanjo na mkewe wakati wakielekea msibani Morogoro, Mzee Ben aliinama kwa uchungu na kuanza kulia kwa kumpoteza rafiki yake,Baadaye waliondoka pamoja hadi hospitalini kwenda kumtizama Mama Joyce anaendelaje walipofika walimkuta amezinduka lakini alikuwa haongei chochote muda wote  alikuwa kimya na alimshangaa kila aliyekuwa anamuona Joyce aliyekuwa karibu na mama yake alimuita “mama, mama mimi mwanao Joyce ongea basi mama hata kidogo” alimuita bila mafanikio mama yake alibaki akimshangaa bila kusema chochote hali ile iliwatatiza sana Mzee Beni na Mama Ngonyani waliokuwa pale hospitalini iliwabidi waende kumuona Daktari ili waweze kufahamu zaidi, ndipo Daktari akawaeleza kuwa mgonjwa amepoteza kumbukumbu zote kwani katika hali aliyonayo hawezi kumkumbuka hata mtoto wake na pia kuna uwezekano hata kama akirudi katika hali yake basi atakuwa hana akili vizuri Mama Ngonyani kusikia hivyo alishtuka na kusema “Mungu wangu sasa itakuwaje ndiyo tumekwisha mpoteza mama Joyce, ina maana Daktari hakuna njia yoyote ya kumrudisha katika hali yake ya kawaida, tusaidie jamani” alizungumza mama Ngonyani huku machozi yakiwa yanamdondoka Daktari alimjibu akisema “Huwezekano hakuna kilichobaki ni Kumuomba Mungu amsaidie pia tunaweza kumruhusu kesho ili muweze kumuhudumia akiwa nyumbani”.



walibaki wanasikitika na kutafakari,  baadaye ilibidi waondoke na kesho yake walirudi kwaajili ya kumchukua mama Joyce ambaye alikuwa haelewi chochote.Maisha yalianza kubadilika kwa mtoto Joyce aliyekuwa na Malengo ya kusoma na baadaye kuwa Mwanasheria hali ilizidi kuwa ngumu kwani Mama Joyce alikuwa akihitaji huduma wakati wote ilifikia kipindi familia ya Mzee Ngonyani ikaanza kuwatenga na hata waliokuwa  marafiki waliwaacha wakitaabika wenyewe, Kutokana na hali kuwa mbaya  Joyce aliamua  kuacha masomo akiwa darasa la sita ili aweze kumsaidia mama yake pale nyumbani Mzee Ngonyani na Mkewe waliamua kuhama katika ile nyumba na tokea walipohama hawakuwahi kurudi hata siku moja kwenda kumsalimia mama Joyce, hali ilizidi kuwa mbaya Joyce na mdogo wake ilibidi wakati mwingine waende mitaani na kuomba msaada angalau wapate pesa ya kula pale nyumbani.



Siku moja Mama Joyce aliamka asubuhi kichwa kilikuwa kinamuuma sana hivyo alitakiwa apelekwe hospitali ambapo Joyce alikuwa hana chochote kwani alikuwa akitegemea biashara ya kuuza maandazi na pesa ilikuwa ni ndogo alihangaika sana bila kupata msaada wowote hatimaye Mama Joyce alifariki Dunia kutokana na kuumwa sana bila kupata matibabu, Aliwaacha  Joyce na James ambao sasa walikuwa ni yatima maisha yalikuwa magumu  hawakujua nini cha kufanya kwani hata nyumba waliyokuwa wakiishi walifukuzwa kutokana na kushindwa kulipa kodi, hivyo kujikuta wakirandaranda mitaani kutafuta kipato…… nini kitatokea huko mitaani na nini hatma yao usikose sehemu ya 4

Post a Comment

Previous Post Next Post