Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Teknoleo

Tumia simu yako kutokomeza wizi tambua kitu chako kilipo

Wataalam wa teknolojia wamegundua njia ambayo inaweza kuwa mwarubaini wa watu kutopoteza vitu vyao kirahisi kwa kuvibaini popote vilipo kwa kutumia simu za kisasa (Smartphone). Teknolojia mpya iliyopewa jina la  TrackR  itawasaidia zaidi watu wengi waliokuwa wanashindwa kujiunga na huduma mbalimbali za kuwekea ulinzi vyombo vyao vya usafiri (track) ili kubaini vilipo, kwa kuzingatia kuwa mtu huhitaji kulipia gharama za kila mwezi kwa huduma hiyo inayotolewa na makampuni mbalimbali yanayotumia mfumo wa ‘GPS’. Kampuni moja imebuni kifaa kinachofahamika kama Track R kinachouzwa kwa bei ambayo watu wengi wenye uchumi wa chini wanaweza kununua, kinachounganishwa na simu ya kisasa ya mtumiaji husika. Mtumiaji anapaswa kufunga kifaa hicho kidogo kwenye kitu anachotaka, kisha ata-download application ya ‘Track R’ kwenye simu yake ya mkononi ya (iPhone au Smartphone) na kuiunganisha na kifaa hicho. Baada ya kukamilisha utaratibu huo, simu yake itakuwa na uwezo wa kumueleza mahali popo

Video: Polisi wa Roboti Apiga Doria Mitaa Ya Dubai, Anaongea Lugha Tisa

Teknolojia inaendelea kuziweka rehani baadhi ya kazi zinazofanywa na idadi kubwa ya binadamu, ambapo jana Dubai imezindua rasmi roboti ya polisi iliyoanza kufanya kazi mitaani ikiwasaka wahalifu na kupokea ripoti. Roboti hiyo iliyofungiwa mfumo wa kielekroniki na kompyuta inaweza kurekodi picha za video na kuzituma kwenye vituo vya polisi, kupanga faini, kubaini sura za watu, huku ikizungumza lugha tisa tofauti. Serikali imesema imebaini kuwa mfumo huo wa kutumia roboti ni mzuri na kwamba kufikia mwaka 2030 mfumo wa roboti utachukua asilimia 25 ya jeshi la polisi. Hata hivyo, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma bora wa Polisi Dubai, Brig Khalid Al Razooqi amesema kuwa roboti haitachukua nafasi ya binadamu katika vitengo vya polisi. “Nafasi za Polisi hazitachukuliwa na roboti. Lakini kwakuwa idadi ya watu wa Dubai inaongezeka, tunahitaji kuwapangia maafisa wa polisi maeneo mengine ili wajikite katika kuhakikisha hali ya usalama kwenye jiji,” alisema Razooqi. Aliongeza kuwa w