Skip to main content

Simu Janja Mpya Kutoka Infinix: Jua Sifa Za Infinix S5!

Hivi unalikumbuka tolea la S4 kutoka simu za Infinix?  Naam! Ni moja kati ya yale matoleo yanayotoka katika  ‘S Series’ . Hivi Sasa kampuni ya Infinix inakuletea toleo lingine linalojulikana kama Infinix S5. Simu hii imekuja sambamba na msimu wa sikukuu hivyo tegemea promoseni ambayo ina zawadi kedekede kutoka kwao Infinix

Ijulikane kwamba kwa sasa Infinix S5 ndio kinara wa matoleo ya ‘S Series’ kutoka Infinix, simu janja hii ina vipengele vya kuvutia kama vile ‘Infinity-O Display’ na Megapixel (MP) 32 katika kamera yake ya selfi.
“Infinix ikiwa ni kampuni yenye ushawishi mkubwa katika mfumo wa kidigitali tunawahakikishia wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei Rafiki”- alisema afisa mahusiano Infinix, Aisha Kurupa
Timu Ya Infinix Ikizindua Simu Janja Ya Infinix S5
Timu Ya Infinix Ikiwa Kazini
SIFA ZAKE KWA UFUPI
  • Kamera ya selfi ambayo ina MP 32
  • Kamera nne za nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens vile vile zikiwa na teknolojia ya Artificial Inteligency (AI)
  • Memori ya uhifadhi wa ndani ni Gb 64 na RAM ni GB 4 kwa ujazo huu simu yako haitawahi kujaa mafaili kwa haraka ila ikitokea unaweza ukaongezea memori kadi ya nje.
  • Betri yake ina ujazo wa mAh 4,000. Ujazo huu utaiwezesha simu janja hii kukaa na chaji kwa muda mrefu sana.
Timu Ya Infinix Ikizindua Simu Janja Ya Infinix S5
Timu Ya Infinix Ikizindua Simu Janja Ya Infinix S5
Infinix S5 ina sifa nyingi sana, pia inakuja katika muonekano wa kitofauti sana wenye kuvutia kutokana na namna kamera ya mbele ilivyopachikwa ndani ya Display kwa jina la kitaalamu Infinity-O Display. S5 pia inakuja na uwezo wa laini mbili za simu zile ndogo kabisa.

Ukiachana na hayo Infinix wametumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi promosheni ya msimu wa sikukuu inayoenda sambamba na uzinduzi wa Infinix S5.
Akizungumza meneja wa mauzo wa Infinix Bwana Fredy Kadilana alisema kwamba, “katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya Infinix imezindua rasmi promotion itakayompa nafasi mteja wa Infinix S5 au mteja wa simu yoyote ya Infinix kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio na nyengine nyingi lakini pia Infinix haijasahau wadau wake wa wanaotembelea kurasa ya @infinixmobiletz kwa kuitambulisha challenge ya #S5showitoff itayoanza rasmi mwishoni mwa wiki hii”.
Muonekano Wa Infinix S5 Ndani Ya Boksi
Kwa maelezo zaidi tembelea www.infinixmobility.com

Ningependa kusikia kutoka kwako, hili kutoka Infinix umelipokea vipi? niandikie hapo chini sehemu ya maoni. Pia Usisit kutemnelea katika mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari kedekede za sayansi na teknolojia kwa ujumla.

Popular posts from this blog

DOWNLOAD; nyimbo mpya ya alikiba #JOHOTENA

Jinsi ya ku-track simu yako na kujua mahali ilipo

Upotevu wa simu yako ni moja ya jambo baya watu wanalipata.Unaweza kuibiwa simu yako iliyokuwa imehifadhi data nyingi binafsi. Kwa msaada jinsi ya kupata simu yako iliyopotea, Google na Apple kwa pamoja wana njia za kufuatilia hili kutafuta mfumo wa simu yako. Jinsi ya kutafuta iPhone iliyopotea Ufumbuzi wake upo kwenye Find My iPhone.Huduma hii ina uwezo wa kukuonyesha kifaa chako chochote cha iOS Kupata uwezo juu ya iPhone yako,fuata hatua hizi; 1.Nenda kwenye setting/mpangilio wa iPhone yako 2.Shuka chini utakuta iCloud 3.Katika chini ya orodha bonyeza "Find My iPhone" 4.Kwenye Find My Phone switch on position 5.Ukiwa hapo ni wazo zuri ku-turn on send last  location Baada ya kuwezesha Find My iPhone,unaweza kuifuatilia vizuri simu yako iliyopotea na kuibiwa Jinsi ya kupata Android phone Kwa android ni tofauti kidogo na Apple.Google wameweka app yao kwenye Play store  na unaweza ku-download 1.Search Play Store "Android Device Manager" 2.Inst

Tumia simu yako kama mounse ya komputa

New Trick Habari za wakati huu msomaji wa Blog yako pendwa ya  DODY BLOG ! Katika mfululizo wa makala za wiki hii, leo tutaangalia jinsi ya  KUTUMIA   simu yako hio ya  SmartPhone kama  Mouse  ya kompyuta. FAIDA >>>Hii inaweza kukusaidia pale ambapo hauna Mouse kwa ajili ya compyuta yako, au  TouchPad  ya Laptop yako haifanyi kazi! Yani  inasumbua! MAHITAJI >> Utahitajika kuinstall program na App ntakazokupa hapa chini! Unaweza kutumia Apps mbalimbali na step ni hizihizi.  Host file utaiinstall kwenye kompyuta yako na App utaiweka kwenye simu yako, halafu utaunga compyuta yako kwenye wireless ya simu yako au bluetooth!  (Lengo la kuunga ni kuweka mawasiliano kati ya simu na kompyuta). kwa hio unaweza kutumia  Bluetooth au Wireless!  Zote ni sawa ila hapa nitaelezea Wireless. HATUA KWA HATUA 1.   Download na install  Monect  kwenye simu yako  HAPA! Install Monect Portable 2. Kwenye PC yako download na install  Monect Host  kwa kuclik  HAPA