Wakati huu ambao kila mtu anapambana nahali yake, ujasiriamali umekua kimbilio la vijana wengi, kama tunavyojua hakuna mtu anaeanzisha kitu kwa lengo la kufeli , japo sio wote hufanikiwa. Leo nawaletea sifa 4 za wajasiriamali waliofanikiwa na pengine ukiziiga, unaweza kuongeza nafasi ya kufanikiwa katika mishe zako.
1. PENDELEA KUAMKA MAPEMA
Huwezi fanikisha malengo yako kama wewe ni mtumwa wa usingizi. siku zote pendelea kuamka mapema ili uweze kukamilisha kazi zilizobaki au ngumu ambazo unatakiwa uzikamilishe kwa siku husika maana akili yako inakuwa bado ina nguvu ya kufanya mambo mengi na kwa ufanisi wakati wa asubuhi. mabilionea wengi duniani ikiwemo Mo Dewji, Bakhlesa, Dangote n.k. wana tabia ya kuamka mapema
2. PANGA SIKU YAKO MAPEMA
Ni vizuri kupangilia siku yako mapema ili kujua uamkapo utaanza na nini. Hii husaidia kazi zako kufanyika kwa mpangilio na kuokoa muda ambao utaruhusu akili yako kufanya kazi na kuvumbua vitu vya nyongeza. Pia itapelekea kuboresha biashara yako na malengo yako uliyojiwekea kutimia
3.THAMINI MUDA WAKO
Ni afadhali upoteze pesa kwa kua utapata nyingine lakini ukipoteza muda ndo basi tena. Watu wote waliofanikiwa wanathamini sana muda, ni vizuri kujua kila saa likipita umefanya kitu gani kinachopelekea kufikia malengo yako.Kumbuka kila siku ni kama akaunti ya benki na muda ni kama pesa zako.Hakuna tajili wala masikini, wote tna masaa 24
4. JIFUNZE KILA SIKU
Hakikisha haipiti siku bila kujifunza kitu kipya. Jifunze kupitia vitabu, internet, semina , changamoto na fursa unazozipata kwenye mishe zako, wateja washindani na hata washauri unaokutana nao.Maisha yako yawe darasa la kuvuna kitu kipya cha kukuleta mafanikio. Kumbuka kujifunza kutaongeza uwezo wako wa kufikiri na kuona mbali.
Post a Comment