-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema nchi yake inapinga vikali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kufungua uchunguzi dhidi ya uhalifu unaotuhumiwa kufanywa na Israel
-
Pompeo amesema, hatua hiyo iliyotangazwa jana na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC inatafuta njia za kuielenga Israel katika namna isiyo ya Haki
-
Uamuzi huo wa ICC wa Madai ya Uhalifu wa Kivita katika eneo la Palestina umezusha majibu ya hasira kutoka Israel ambapo Wapalestina wameukaribisha uamuzi huo na kusema umechelewa kufuatia uchunguzi wa awali wa karibu miaka 5 tangu kuzuka kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza 2014
-
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameutaja uamuzi wa Mahakama hiyo ambayo Israeli ilikataa kujiunga nayo tangu ilipooundwa mwaka 2002, kuwa ni "Silaha ya Kisiasa" dhidi ya Taifa hilo la Kiyahudi
-
Hata hivyo, Netanyahu amesema Mahakama ya ICC haina uwezo wa kuchunguza yanayotokea ndani ya mipaka ya Palestina