Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kwamba Paul Pogba "hatauzwa Januari" na pia amekanusha madai ya kwamba amekutana na mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland jana siku ya Ijumaa.
Pogba, kiungo huyo wa kati wa United, amerejea baada ya kupata jeraha lakini pia amekuwa akihisi vizuri na kuna uwezekano mkubwa asicheze katika mechi dhidi ya Watford Jumapili ijayo.
Wakati huo huo, kuna taarifa zinazodai kwamba Haaland amesafiri kutoka Stavanger Norway hadi Manchester na babake.
Lakini Solskjaer amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ni "zawadi ya Krismasi". "Sidhani kama hatma yake ni hapa, amesema. "Siwezi kuzungumzia wachezaji wa timu nyengine. watu wataanza kuwa na mashaka na wewe." Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba alikuwa anatarajiwa kurejea katika kambi ya mazoezi wiki iliyopita baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguuni ambalo limemfanya kuwa nje tangu Septemba lakini akauguwa na hali yake ikawa inaendelea kuwa mbaya Jumapili iliyopita.
Hata hivyo, Solskjaer amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anakaribia kurejea na hataondoka Old Trafford mwezi ujao. "Hatauzwa Januari,"amesema maneja wa United. "Ni matumaini yangu kwamba ataingia uwanjani kabla ya mwisho wa mwaka huu, lakini sitamlazimisha. Siwezi kujiweka katika hatari ya kupata changamoto au wachezaji wangu kupata jeraha."