MOROGORO: AKAMATWA AKIWA UCHI NA MTOTO MTONI

Mtu mmoja (Jina halijafahamika) anashikiliwa na Polisi baada ya kukutwa mtoni na mtoto mwenye umri kati ya miaka 5 na 10, wote wakiwa hawana nguo huku akiwa na panga na msumeno
-
Tukio hilo limetokea Desemba 19, 2019 katika Maporomoko ya Maji ya Nguzi Camp, na taarifa zinaeleza kuwa wakati mtu huyo akiwa katika Maporomoko hayo, Askari waliokuwa katika shughuli nyingine walimuona na kumtilia shaka
-Related image
Inadaiwa kuwa, baada ya kuonekana alijitosa kwenye maji ya kina kirefu akiwa na mtoto huyo ambaye alikuwa akipiga kelele na kusema “baba unaniua, baba unaniua”
-
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amesema atalitolea maelezo ya kina tukio hilo leo Jumamosi Desemba 21 katika mkutano na Waandishi wa Habari

Previous Post Next Post