Jumamosi ya March 4 2017 katika Ligi Kuu England ilichezwa michezo kadhaa lakini usiku wake ndio ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu mchezo kati ya majogoo wa jiji la Liverpool dhidi ya Arsenal The Gunners wa London.
Arsenal ambao leo wameripotiwa kumtafuta mbadala wa Wenger kutokea Juventus, wamejikuta wakikutana na kipigo cha goli 3-1, Liverpool wamewafunga Arsenal wakiwa kwao na kufanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 52 na Arsenal wakifanya hivyo kwa silimia 48.
Magoli ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino dakika ya 9, Sadio Mane dakika ya 40 na Georginio Wijnaldum dakika ya 90, wakati goli pekee la Arsenal lilipatikana dakika ya 57 kupitia kwa Danny Welbeck, matokeo hayo yanaifanya Arsenal kushuka hadi nafasi ya 5 wakiwa na point 50, huku Liverpool wakipanda hadi nafasi ya tatu kwa point 52.
Post a Comment