Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2017

VIDEO; alikiba amzungumzia baraka da prince

Alikiba - Seduce Me (Official Music Video)

TETESI ZA USAJILI ULAYA MAHREZ KWENDA MAN U

Bado masaa yasiyozidi 40 ili dirisha la usajili barani Ulaya kufungwa, kila timu inajaribu kupata sahihi ya mtu sahihi kwa ajili ya msimu huu wa ligi na matumizi makubwa ya pesa yanafanya muda huu uliobaki kuwa wa kuvutia. Thomas Lemar ambaye alikuwa anatajwa kuelekea Anfield kukipiga na klabu ya Liverpool inaonekana Barca wameingilia kati usajili huo na sasa wanataka kumnunua Lemar, taarifa zinadai Barca wanapambana kuipiku Liverpool ndani ya usiku wa leo au kesho. Oxlade Chamberlain naye amekuwa akizungumziwa sana hii leo, Chamberlain alikuwa akihusishwa kuelekea Stamford Bridge na inasemekana Chelsea walishakubali kutoa £35m ili kumnunua lakini leo habari mpya zinadai Chamberlain amekataa kujiunga na Chelsea na anataka aende Liverpool. Angel Di Maria anaweza kurudi tena katika ligi kuu ya Hispania La Liga, lakini kubwa zaidi ni kwamba safari hii Di Maria anarudi Hispania ambako anatakwa na wapinzani wakubwa wa timu yake ya zamani Real Madrid ambao ni Barcelona, taarif

Maneno ya alikiba baada ya kutajwa kama vijana 100 wa afrika wenye ushawishi

Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Alikiba kutajwa kuingia katika orodha ya vijana 100 wenye ushawishi Afrika 2017, ameelezea furaha yake. “Najisikia vizuri kwamba Africa nzima imekutambua, kuna watu ambao wanatamani kuwa kama Alikiba na vitu kama hivyo. Kwa hivyo nawahamasisha vijana wengine kufanya kazi nzuri kama mimi nivyofanya, nashukuru sana, najisikia vizuri,” ameiambia The Playlist ya Times Fm. Vijana wengine wa kitanzania waliotajwa katika orodha hiyo iliyotolewa na African Youth Awards  ni pamoja na Nancy Sumari, Diamond Platnumz, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Flaviana Matata, Millard Ayo na Jokate.

Lipumba ampigia magoti Maalim Seif amtaka arudi wayamalize ila kwa kumsikiliza mwenyekiti

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti. Profesa Lipumba amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya ofisi za Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo Buguruni, Lipumba amemtaka Katibu Mkuu huyo kurudi wafanye mazungumzo na atambue kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa CUF na ndiye boss wake. "Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze"

Bomoa bomoa dar yaipitia nyumba ya mkapa

TAARIFA RASMI YA CHAMA CUF JUU YA KUTOKA MAHAKAMANI LEO TAREHE -15/8/2017:

1. SHAURI LA WABUNGE 8 WA CUF NAMBA 479/2017 MAHAKAMA KUU IMEPANGA KUTOA MAAMUZI YA MAOMBI YA ZUIO LA MUDA KESHO SAA 7:30 MCHANA.  2. WALINZI WA CUF WALIOSINGIZIWA KUWA NA SILAHA NA VIRIPURISHI WASHINDA KESI MAHAKAMA YA KISUTU. 3. ORODHA YA MASHAURI YALIYOPO MAHAKAMANI MWEZI AUGUST, 2017. Mbele ya Mheshimiwa Jaji LUGANO MWANDAMBO leo amesikiliza hoja za Mapingamizi ya awali (Preliminary Objection) yaliyowekwa na Lipumba na wenzake na Attorney General-AG katika shauri la Madai namba 479/2017 dhidi ya Lipumba na wenzake 14 akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi NEC, na Katibu wa Bunge, upande wa Wabunge [8] na madiwani [2] umewakilishwa na Wakili Msomi Peter Kibatara. Maombi hayo yaliyofunguliwa Tarehe 4 August 2017 na kupangwa kusikilizwa leo Tarehe 15 August, 2017. Msingi wa mapingamizi hayo ni mrejeo wa yaleyale ya awali ambapo walidai kuwa Mahakama haina mamlaka ya kutoa Amri ya Zuio kwa Bunge na kwamba vifungu vilivyonukulwa na kuwekwa katika maombi hayo si sahihi.

Kizungumkuti chaibuka Chelsea, Conte kuondoka, Costa kubaki

Hali ya sintofahamu imezidi kuiandama klabu ya Chelsea, kumekuwa na matukio ambayo hayaeleweki toka msimu umeisha lakini kipigo cha juzi kutoka kwa Burnley kimezidi kuchafua hali ya hewa ndani ya Chelsea. Kama unakumbuka wiki chache baada ya dirisha la usajili ndani ya Chelsea kufunguliwa kuliibuka tetesi kwamba Antonio Conte amechukizwa na sera za usajili wa Chelsea hali iliyofikia kutaka kuondoka. Moja ya malalamiko ya Conte ilikuwa ni kukosa userious katika suala la usajili jambo ambalo lilipelekea kukosa wachezaji awatakao akiwemo Romelu Lukaku na pia Conte akitaka kupewa nafasi kubwa zaidi katika maamuzi. Maisha yakaendelea na Conte akasaini mkataba mpya lakini wiki hii suala hilo limejitokeza tena na taarifa zinasema hali sio shwari hata kidogo kati ya klabu ya Chelsea na Muitaliano huyo baada ya Conte kudai mabosi wanamuangusha. Wachambuzi mbali mbali wa masuala ya soka barani Ulaya wameshaanza kutabiri kwamba huu ni msimu wa mwisho wa Conte huku wacheza kamari nao

Costa atishia kuigomea Chelsea mwaka mzima

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, ameanzisha mashambulizi dhidi ya kocha wake Antonio Conte na klabu yake kwa jumla wakati akiwa mji wa nyumbani kwake nchini Brazil.Mpachika mabao huyo mwenye miaka 28, amemkosoa Conte kwa kitendo chake cha kumtumia ujumbe mfupi wa simu mapema katika msimu huu wa kiangazi uliomjuza kuwa mwanandinga huyo haitajiki tena  klabuni hapo.Costa anaamini kuwa vijana hao wa darajani, wanazuia mahaba yake ya kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid na kusema kuwa anajiandaa kutundika daruga na kwenda kukaa Brazil kwa mwaka mzima bila kucheza, hata kama timu hiyo itamwadhibu.Akizungumza na baadhi ya magazeti ya nchini Uingereza, Costa amesema “mwezi Januari mambo yaliyotokea ni kutokana na kocha, nilikuwa kwenye kipindi cha kuuhisha mkataba wangu na wakasitisha jambo hilo,” alisema Costa.“Nadhani kwamba kocha alikuwa nyuma ya hayo, aliomba jambo hilo litokee, nimemwona ni aina gani ya mtu, ana mtazamo wake na hilo halitobadilika, namuheshi

Viingilia mechi ya ngao ya hisani kati ya simba na yanga vyatajwa

Shirikisho la soka Tanzania leo limetangaza viingilio katika mchezo wa ngao ya jamii utakaowakutanisha mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara 2016/17, Young Africans na mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam, Simba.Viingilio katika mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam vimepangwa katika makundi manne kama ifuatavyo.Sehemu ya VIP ‘A’ tiketi zake ni shilingi 25,000; sehemu ya VIP ‘B’ na ‘C’ shilingi 20,000; viti vya rangi ya chungwa shilingi 10,000 na mzunguko kwa viti vya rangi za bluu na kijani ni shilingi 7,000.Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika shirikisho hilo, tiketi zimeanza kuuzwa leo Jumanne Agosti 15, 2017 ili kuwapa fursa wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi mapema kujiepusha na usumbufu

Simba, yanga uso kwa uso visiwani Zanzibar

Mabingwa wa FA, klabu ya soka ya Simba jioni ya leo inataraji kusafiri kwenda Visiwani Zanzibar kuweka kambi kwaajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Dar es salaam Young Africans utakao pigwa Agosti 13 mwaka huu. Kikosi cha Timu ya Simba Timu hiyo inakwenda Zanzibar kujiwinda na mchezo huo huku watani zao wa jadi Yanga wakiwa tayari wamesha wasili Visiwani humo mara baada ya kucheza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting. Simba ambayo imedhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa inaonekana kufanya vizuri katika usajili wake msimu huu kwa kuwasajili baadhi ya wachezaji golikipa Aishi Manula , beki Shomari Kapombe, mshambuliaji John Bocco wote kutokea Azam FC, Ammanuel Mseja, Ally Shomari, Saidi Mohamed, Haruna Niyonzima huku wa kifanikiwa kumrudisha mchezaji kipenzi cha mashabiki wa msimbazi Emmanuel Okwi. Mbali na mchezo dhidi ya Yanga lakinipia klabu hiyo itatumia kambi hiyo kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania Bar

Ronaldo kukosa michezo 12

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo huenda akafungiwa mechi 12 kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu alichokifanya kwa muamuzi, Ricardo De Burgos katika mchezo wao dhidi ya Barcelona Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, alimsukuma muamuzi, Ricardo De Burgos raia wa Hispania baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza Supercopa de Espana ambao Madrid ilichomoza na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wa Camp Nou. Kutokana na sheria ya soka nchini Hispania kifungu cha 96 kinatumika kwa wachezaji wasio na utovu wa nidhamu kwa kitendo cha kumsukuma muamuzi, kumvuta ama kumtikisa kwa makusudi pindi awapo mchezoni kukabiliwa na adhabu ya kukosa michezo kati ya minne hadi 12.