Skip to main content

Lipumba ampigia magoti Maalim Seif amtaka arudi wayamalize ila kwa kumsikiliza mwenyekiti

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti.



Profesa Lipumba amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya ofisi za Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo Buguruni, Lipumba amemtaka Katibu Mkuu huyo kurudi wafanye mazungumzo na atambue kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa CUF na ndiye boss wake.

"Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze" alisisitiza Lipumba

Aidha Lipumba amesema kama Katibu Mkuu wa CUF hatakuja ofisini kwa ajili ya majadiliano na mazungumzo kwa lengo la kumaliza migogoro yao basi Naibu Katibu Mkuu ataendelea kukaimu nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba yao ya CUF.

"Katibu Mkuu akishindwa kutekeleza majukumu yake Naibu Katibu Mkuu anafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya Mwenyekiti ataendelea Kukaimu nafasi hiyo mpaka pale Katibu Mkuu atakapokuwa tayari kuja hapa ataruhusiwa kufanya kazi na ofisi yake ipo hapa, akiwa anakuja ofsini anafuata utaratibu na kufuata maelekezo yangu mimi sina shida ila kama hatakuja basi Naibu Katibu Mkuu ataendelea kufanya kazi" alisema Lipumba


Mbali na hilo Lipumba amesema kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) toka kimempokea Mhe. Edward Lowassa wameacha ajenda ya ufisadi na wameiweka kando ajenda hiyo na kusema sasa hivi wao ndiyo ajenda yao hiyo

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD; nyimbo mpya ya alikiba #JOHOTENA

Jinsi ya ku-track simu yako na kujua mahali ilipo

Upotevu wa simu yako ni moja ya jambo baya watu wanalipata.Unaweza kuibiwa simu yako iliyokuwa imehifadhi data nyingi binafsi. Kwa msaada jinsi ya kupata simu yako iliyopotea, Google na Apple kwa pamoja wana njia za kufuatilia hili kutafuta mfumo wa simu yako. Jinsi ya kutafuta iPhone iliyopotea Ufumbuzi wake upo kwenye Find My iPhone.Huduma hii ina uwezo wa kukuonyesha kifaa chako chochote cha iOS Kupata uwezo juu ya iPhone yako,fuata hatua hizi; 1.Nenda kwenye setting/mpangilio wa iPhone yako 2.Shuka chini utakuta iCloud 3.Katika chini ya orodha bonyeza "Find My iPhone" 4.Kwenye Find My Phone switch on position 5.Ukiwa hapo ni wazo zuri ku-turn on send last  location Baada ya kuwezesha Find My iPhone,unaweza kuifuatilia vizuri simu yako iliyopotea na kuibiwa Jinsi ya kupata Android phone Kwa android ni tofauti kidogo na Apple.Google wameweka app yao kwenye Play store  na unaweza ku-download 1.Search Play Store "Android Device Manager" 2.Inst

Tumia simu yako kama mounse ya komputa

New Trick Habari za wakati huu msomaji wa Blog yako pendwa ya  DODY BLOG ! Katika mfululizo wa makala za wiki hii, leo tutaangalia jinsi ya  KUTUMIA   simu yako hio ya  SmartPhone kama  Mouse  ya kompyuta. FAIDA >>>Hii inaweza kukusaidia pale ambapo hauna Mouse kwa ajili ya compyuta yako, au  TouchPad  ya Laptop yako haifanyi kazi! Yani  inasumbua! MAHITAJI >> Utahitajika kuinstall program na App ntakazokupa hapa chini! Unaweza kutumia Apps mbalimbali na step ni hizihizi.  Host file utaiinstall kwenye kompyuta yako na App utaiweka kwenye simu yako, halafu utaunga compyuta yako kwenye wireless ya simu yako au bluetooth!  (Lengo la kuunga ni kuweka mawasiliano kati ya simu na kompyuta). kwa hio unaweza kutumia  Bluetooth au Wireless!  Zote ni sawa ila hapa nitaelezea Wireless. HATUA KWA HATUA 1.   Download na install  Monect  kwenye simu yako  HAPA! Install Monect Portable 2. Kwenye PC yako download na install  Monect Host  kwa kuclik  HAPA