TAARIFA RASMI YA CHAMA CUF JUU YA KUTOKA MAHAKAMANI LEO TAREHE -15/8/2017:


1. SHAURI LA WABUNGE 8 WA CUF NAMBA 479/2017 MAHAKAMA KUU IMEPANGA KUTOA MAAMUZI YA MAOMBI YA ZUIO LA MUDA KESHO SAA 7:30 MCHANA. 

2. WALINZI WA CUF WALIOSINGIZIWA KUWA NA SILAHA NA VIRIPURISHI WASHINDA KESI MAHAKAMA YA KISUTU. 3. ORODHA YA MASHAURI YALIYOPO MAHAKAMANI MWEZI AUGUST, 2017.
Related image
Mbele ya Mheshimiwa Jaji LUGANO MWANDAMBO leo amesikiliza hoja za Mapingamizi ya awali (Preliminary Objection) yaliyowekwa na Lipumba na wenzake na Attorney General-AG katika shauri la Madai namba 479/2017 dhidi ya Lipumba na wenzake 14 akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi NEC, na Katibu wa Bunge, upande wa Wabunge [8] na madiwani [2] umewakilishwa na Wakili Msomi Peter Kibatara. Maombi hayo yaliyofunguliwa Tarehe 4 August 2017 na kupangwa kusikilizwa leo Tarehe 15 August, 2017. Msingi wa mapingamizi hayo ni mrejeo wa yaleyale ya awali ambapo walidai kuwa Mahakama haina mamlaka ya kutoa Amri ya Zuio kwa Bunge na kwamba vifungu vilivyonukulwa na kuwekwa katika maombi hayo si sahihi.

AMRI YA MAHAKAMA KUU; 
1. Mahakama imeamuru mapingamizi yote yasikilizwe kwa nja ya maandishi (Written Submission) na uamuzi (Ruling) itatolewa Tarehe 27 August, 2017. Kwa ratiba ya uwasilishaji iliyowekwa. 2. Mahakama pia iliombwa na Wakili Msomi Peter Kibatala kutoa Zuio la muda (Temporary Injunction) ili kubakisha hali ilivyo sasa mpaka pale mapingamizi yatakapoamuliwa (Maintenance of Status Quo). Mahakama itatoa uamuzi juu ya hilo kesho Tarehe 16 August, 2017 saa 7.30 mchana. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Viongozi na Wanachama wote walojitokeza kwa wingi kuskiliza shauri hili Mahakamani.

WALINZI WA CUF 22 WALIOBAMBIKWA KESI NA LIPUMBA AKISHIRIKIANA NA VYOMBO VYA DOLA WAMEISHINDA JAMHURI NA KUACHIWA HURU:

LEO Katka mahakama ya Kisutu Dar es salaam, Mheshimiwa hakimu Mwambapa ameifuta kesi ya Jinai namba 354 ya mwaka 2016 chini ya Sheria namba 225 ya makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act) kesi hiyo iliyowahusu walinzi wa Chama 22 waliokamatwa wakiwa katika Bus aina ya Coaster wakielekea Buguruni ghafla walizingirwa na Gari ya Polisi kwa Taarifa zilzotolewa na ‘Mungki’ kwa Jeshi la Polisi na kukamatwa vijana wote 22 [Blue Guards] na kufikishwa kituo kikuu cha Polisi [Central polisi] ambapo walilazwa ktuoni hapo kwa zaidi ya siku 7 na kisha kufikishwa Mahakama ya Kisutu walipofunguliwa mashtaka ya 1. Kula njama za kutenda kosa. 2. Kuingilia na kutekeleza majukumu ya Jeshi la Polisi na 3. Kukutwa na Viripurishi, silaha na kemikali za sumu. (yaani makopo ya dawa ya mbu ya Rungu, kisu) Kufutwa kwa kesi hiyo kumetokana na Jamhuri kushindwa kuwasilisha maelezo ya awali na kuithibitishia mahakama kosa la washtakwa kwa takribani kipindi cha miezi 11 toka walipokamatwa Septemba, 2016.

Katika hairisho la mwisho la kesi hiyo Hakimu Mwambapa aliieleza Jamhuri kuwa endapo ikishindwa kuleta ushahidi ataifuta kesi hiyo na ndivyo ilivyofanyika leo. Washtakiwa hao walikuwa wanatetewa na Wakli Msomi Hashimu Mziray, ambae pia n Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) Upande wa Jamhuri uliwakishwa na Wakili Msomi Nassoro Katuga.

JARIBIO LA KUTAKA KUWAKAMATA TENA LASHINDIKANA: 

Mara baada ya kuachiwa huru kuna watu waliokuwepo mahakamani hapo ambao wamevaa mavazi yanayofanana na sare za Jeshi la Polisi walitoa amri ya kukamatwa tena ambapo mapambano makali yalitokea na kufanikiwa kuwakamata 4 kati ya 22 ndani ya chuma cha Mahakama wakati hakimu akiwepo jambo ambalo ni kosa kisheria. Sheria inakataza mtu kukamatwa mbele ya Hakimu hata akiwa amefanya kosa au fujo ya namna gani mpaka pale Amri ya kukamatwa itoke kwenye kiti cha Hakimu.

MADHIRA WALIYOKUTANA NAYO KATIKA KADHIA HII: 

Walinzi wetu kwanza walikatwa na kuwekwa sero kwa siku zaidi ya 7 na ksha kupelekwa mahakamani na baadae kukosa dhamana na kupelekwa Gereza la Segerea kama Mahabusu. Walilazimika kuwa mbali na familia zao, kuharibikiwa shughuli na biashara zao, kutuma fedha kugharama safari za kufika mahakamani mara kwa mara wengne kutoka Unguja, Zanzibar takiribani zaidi ya safari 36 kwenda na kurudi na kadharika.

Jeshi la Polisi lilituma nguvu kubwa kutangaza kukamatwa kwa watu wenye Silaha na VIRIPURISHI/MABOMU na kuchafuliwa majina yao katika mitandao ya kijamii. Walibezwa na kukashifiwa na kundi la WASALITI WA BUGURUNI wakiwa wao ndio walioshiriki kufanya hivyo siku chache kabla ya uvamizi wa Ofisi Kuu ya Buguruni mwaka jana Tarehe 24/9/2016.Leo Jamhuri iliyokuwa na kishindo hicho imeshindwa kuthibitisha TUHUMA ZAKE DHIDI YAO na kesi imefutwa kwa kuondolewa kirahisi kabisa. Hii ndio serikali inayotetea Wanyonge inayojigamba kutenda Haki, Msema kweli mpenzi wa Mungu. 

HAKUNA KURUDI NYUMA, MAPAMBANO LAZIMA YAENDELEE.

RATIBA YA MASHAURI YALIYOPO MAHAKAMANI AUGUST, 2017 MPAKA SASA: 

1. KESHO Tarehe 16/8/2017 – maamuzi ya shauri namba 479/2017 la Wabunge kuhusu Zuio. 2. Tarehe 17/8/2017 – shauri namba 477/2017 la Ally Salehe na Bodi ya Wadhamini ya RITA, Lipumba na wenzake. Maombi ya Zuio. Pingamizi llilowekwa na Lipumba na wenzake linasikilizwa.

Msikose kuja kupata Burdani ya kisheria Toka kwa Wakili Msomi Fatuma Karume na Mpare Kabe Mpoki. 3. Tarehe 18/8/2017 Mahakama YA Rufaa Tanzania- Shauri namba 43/2017 kuomba muda (extension of Time) kuingiza Rufaa kumkataa Jaji KIHIYO. Lakini ndio ameshastaafu sasa. Tutajulishana. 

4. Tarehe 22/8/2017 Shauri la Msingi (Civil Case No. 13/2017) kuhusu uhalali wa Bodi ya RITA- Ally Salehe dhidi ya Lipumba na wenzake. 5. Tarehe 22/8/2017 Shauri dogo la Madai (Miscelleneous Civil Application No.28/2017) hili linahusiana na Maombi ya Zuio [Injuction] la kusitisha Ruzuku isitolewe kwa Lipumba na Kundi lake. Hakuna fedha ya Ruzuku itakayotolewa mpaka shauri hili litakapofanyiwa maamuzi vinginevyo. Kwa sababu Amri ya Mahakama kuzuia Ruzuku haijatenguliwa.

AMRI YA ZUIO IKO PALEPALE

6. Tarehe 22/8/2017 Shauri la Jinai namba 50/2017 (Contempt of Court Proceedings)-shauri hili dhidi ya Lipumba na wenzake, Emmy Hudson-RITA, jaji Franscis Mutungi linahusiana na kughushi nyaraka na kutaka kuingilia mwenendo wa mashauri yaliyopo mahakamani. 

7. Tarehe 27/8/2017 –Maamuzi (Rulings) ya Pingamizi shauri la Wabunge 8 na madwani 2. 8. Tarehe 31/8/2017 – shauri la Msingi namba 143/2017 Wabunge wa CUF 8 na Madiwani 2. Hii ndio Orodha/ratiba ya Mashauri kwa Mwezi huu, kama kuna mabadiliko na nyongeza Kurugenzi ya habari itawajulisha.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI. HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo Tarehe 15/8/2017 Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa SALIM BIMANI MKURUGENZI

Post a Comment

Previous Post Next Post