Ticker

6/recent/ticker-posts

Costa atishia kuigomea Chelsea mwaka mzima

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, ameanzisha mashambulizi dhidi ya kocha wake Antonio Conte na klabu yake kwa jumla wakati akiwa mji wa nyumbani kwake nchini Brazil.Mpachika mabao huyo mwenye miaka 28, amemkosoa Conte kwa kitendo chake cha kumtumia ujumbe mfupi wa simu mapema katika msimu huu wa kiangazi uliomjuza kuwa mwanandinga huyo haitajiki tena 

Image result for diego costa
klabuni hapo.Costa anaamini kuwa vijana hao wa darajani, wanazuia mahaba yake ya kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid na kusema kuwa anajiandaa kutundika daruga na kwenda kukaa Brazil kwa mwaka mzima bila kucheza, hata kama timu hiyo itamwadhibu.Akizungumza na baadhi ya magazeti ya nchini Uingereza, Costa amesema “mwezi Januari mambo yaliyotokea ni kutokana na kocha, nilikuwa kwenye kipindi cha kuuhisha mkataba wangu na wakasitisha jambo hilo,” alisema Costa.“Nadhani kwamba kocha alikuwa nyuma ya hayo, aliomba jambo hilo litokee, nimemwona ni aina gani ya mtu, ana mtazamo wake na hilo halitobadilika, namuheshimu kama kocha mkubwa, amefanya kazi nzuri hata mimi naweza kuiona, lakini yeye kama mtu nasema hapana,” aliongeza Costa.

Post a Comment

0 Comments