Skip to main content

Posts

ALIKIBA KAYAONGEA HAYA

Ni Interview aliyofanyiwa mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba kwenye kituo cha Radio cha Johannesburg South Africa kiitwacho Trans Africa Radio NET, Alikiba alihojiwa kuhusu ishu mbalimbali zikiwemo za muziki wake na maisha…  hii video hapa chini ina kila kitu. ULIPITWA?  Hii hapa chini ni Full Video ya Alikiba akitumbuiza Durban South Africa wiki iliyopita

RIVER YAINYUKA ARSENAL

Jumamosi ya March 4 2017 katika Ligi Kuu  England  ilichezwa michezo kadhaa lakini usiku wake ndio ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu mchezo kati ya majogoo wa jiji la  Liverpool  dhidi ya  Arsenal The Gunners  wa  London . Arsenal  ambao leo wameripotiwa kumtafuta mbadala wa  Wenger  kutokea  Juventus , wamejikuta wakikutana na kipigo cha goli 3-1,  Liverpool  wamewafunga  Arsenal  wakiwa kwao na kufanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 52 na  Arsenal  wakifanya hivyo kwa silimia 48. Magoli ya  Liverpool  yamefungwa na  Roberto Firmino  dakika ya 9,  Sadio Mane  dakika ya 40 na  Georginio Wijnaldum  dakika ya 90, wakati goli pekee la  Arsenal  lilipatikana dakika ya 57 kupitia kwa  Danny Welbeck , matokeo hayo yanaifanya  Arsenal  kushuka hadi nafasi ya 5 wakiwa na point 50, huku  Liverpool  wakipanda hadi nafasi ya tatu kwa point 52. Msimamo wa Ligi Kuu England ulivyo kwa sasa baada ya kuchezwa mechi za March 4 2017.

HIVI NDIVYO ALIVYOJIBU JOKATE BAADA YA KUULIZWA SWALI KUHUSU FAMILIA YA ALIKIBA

Hivi karibuni Mama wa mwimbaji wa BongoFleva,  Alikiba alidai kuwa anamchukulia  Jokate  kama rafiki wa Zabibu “dada wa Alikiba” na kuhusu kuwa rafiki wa  Alikiba  hajui kwani hajatambulishwa.  Alikiba  naye alipoulizwa alidai Jokate si mpenzi wake bali rafiki yake tu. Leo March 4 2017 kupitia kipindi cha  Clouds 360  cha Clouds TV Mrembo Jokate ameulizwa anachukulia vipi hayo majibu yaliyotolewa na Mama yake Alikiba na Alikiba mwenyewe. Haya ni majibu yake….. >>>  “Unajua katika maisha huwezi kumlazimisha mtu kuona thamani yako, wanasema tenda wema nenda zako mengine ni matokeo na sipendi kulizungumzia sana maana siku hizi watu wanapenda sana kuokota maneno wanayatengeneza wanavyojua wao” >>>”Mimi sifikirii sana maana mimi ni mtu Positive nataka niamini hawakuamaanisha sasa sijui waliteleza au walikosea”

RAFU ALIYOFANYIWA TOREZI HADI KUCHUKULIWA NA AMBURANCE UWANJANI

Staa wa soka wa kimataifa wa  Hispania  anayeichezea  Atletico Madrid,  Fernando Torres usiku wa March 2, 2017 alishtua mashabiki wa soka na wachezaji wenzake kufuatia kupata jeraha kichwani na kufanya kila mchezaji aliyepo uwanjani kushtuka na jeraha hilo. Torres,  ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha  Atletico Madrid  kilichocheza na  Deportivo la Coruna  katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, alilazimika kukimbizwa hospitali na ambulance kufuatia kuumia kichwani na kupoteza fahamu baada ya kugongwa na  Alex Bergantinos  dakika ya 85. Taarifa kutoka Hospitali ambayo staa huyo wa zamani wa  Liverpool  na  Chelsea  aliyezichezea timu hizo kwa nyakati mbili tofauti, amepata fahamu na  Atletico  wameripoti kuwa atakuwa katika uangalizi wa daktari kwa usiku wote huu.

ALICHOKIFANYA RAIS TRUMP BAADA YA KUJUA UWEPO WA CLINTON

Tuliona wakirushiana maneno sana kwenye kampeni zao kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais kwenye taifa la Marekani wakiwa ni Wapinzani wawili, tuliona jinsi ushindi wa  Trump  ulivyostaajabisha mamilioni ambao hawakutarajia kilichotokea. Sasa pamoja na yote hayo, pamoja na  Hillary  kushindwa… yeye na mume wake Bill Clinton walihudhuria kuapishwa kwa  Donald Trump  na baadae kwenye hafla ambapo baada ya Rais Trump kutambua uwepo wao, akaomba watu wote waliomo ndani wasimame, hii video hapa chini ina kila kitu.

tutanchukulia hatua aliyempa makonda kwanja

Lukuvi kumchukulia hatua aliyempa kiwanja Makonda. Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara aliyemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa kuwa eneo hilo sio lake ni mali ya serikali."Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu," alisema Lukuvi. Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara aliyemkabidhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Pau l Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa sababu eneo hilo si lake ni mali ya Serikali. “Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu,”amesema Lukuvi leo (Jumatatu) katika mkutano na waandishi wa habari. Lukuvi amesema anataka watu wote wanaomiliki maeneo mijini kujisalimisha kwa maofisa ardhi wa wilaya wa ajili ya uhakiki. Chanzo: Mwananchi