Staa wa soka wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Atletico Madrid, Fernando Torres usiku wa March 2, 2017 alishtua mashabiki wa soka na wachezaji wenzake kufuatia kupata jeraha kichwani na kufanya kila mchezaji aliyepo uwanjani kushtuka na jeraha hilo.
Torres, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Atletico Madrid kilichocheza na Deportivo la Coruna katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, alilazimika kukimbizwa hospitali na ambulance kufuatia kuumia kichwani na kupoteza fahamu baada ya kugongwa na Alex Bergantinos dakika ya 85.
Taarifa kutoka Hospitali ambayo staa huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea aliyezichezea timu hizo kwa nyakati mbili tofauti, amepata fahamu na Atletico wameripoti kuwa atakuwa katika uangalizi wa daktari kwa usiku wote huu.
Post a Comment