Skip to main content

Posts

Roboti iliyopewa uraia nchini Saudi Arabia imesema kuwa ina haki ya kuwa na familia

Roboti iliyopewa uraia nchini Saudi Arabia imesema kuwa ina haki ya kuwa na familia. Roboti hiyo kwa jina la Sophia  ilitengenezwa nchini Hong Kong na kupewa uraia nchini Saudi Arabia mwezi uliopita. Roboti hiyo İimesema kuwa ingependa kuwa na familia wakati ilipohudhuria mkutano wa habari ulioandaliwa nchini UAE. Kwa mujibu wa habari roboti hiyo imesema kuwa familia ni kitu muhimu sana. Robot hiyo imesema kuwa kila mwanadamu ana haki ya kuwa na familia na watu wenye hisia sawa na yeye.Jambo hilo ni muhimu sana hata kwa roboti.Aliwaambia wanadamu wajisikie furaha kuwa na familia.

TRA kumchunguza Askofu Kakobe baada ya kumsikia akisema ana hela kuliko Serikali

 Kufuatia Kauli ya Askofu Kakobe kusema "Nina hela kuliko Serikali" sasa TRA wapanga kumchunguza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema; Watu wa Kodi (TRA) wanasema wamepokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao TRA wanaendelea na kusema; Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema Hivyo Askofu Kakobe ni tajiri sana kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania TRA wanasema wanawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe wakaanza kupitia kumbuk

Tetesi za usajili ulaya jumamosi tareh 30/12/2017

  Cristiano Ronaldo Cristiano Ronaldo ameitaka klabu ya Real Madrid kuweka bei yao ya kumuuza isiopungua £89m). Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Ureno yuko tayari kuondoka Uhispania.(Daily Record) Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, hajakaataa kuongeza kandarasi na mabingwa hao watetezi wa Uingereza licha ya madai kutoka kwa babake kwamba anataka kuhamia Real Madrid.(Independent)     Eden Hazard Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anajiandaa kumnunua winga wa Ivory Coast na Crystal Palace Zaha ili kuchukua mahala pake mshambulijai wa Chile Alexis Sanchez, 29. (Daily Star) Wachezaji kadhaa wa Arsenal walidaiwa kumshutumu mshambuliaji Alexi Sanchez kwa kuwa na tabia

una simu ya Android ?Soma utafiti huu

Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana. Uchnguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake.   Aidha simu hizo zinaweza kudukuliwa kwa kutumia matumizi ya betri yake huku utafiti ukisema kuwa simu zinazotumika karibu na kifaa cha kupeperushia masafa ya simu za kuungia mbali. Simu za kisasa ''Smartphone'' hutumia nguvu zaidi inapokuwa mbali zaidi na kifaa hicho cha kupeperushia masafa ya GSM, kwani inachangamoto tele za kungamua masafa. Matumizi ya nguvu zaidi ya shughuli zingine yanaweza kubaiishwa na ''alogarithm'' muundo msingi wa simu yenyewe. Watafiti hao sasa wameunda mfumo ambao unakusanya habari kuhusu matumizi ya betri ya simu. ‘’Mfumo huo hairuhusu kutumia GPS wala huduma zozote kwa mfano mtandao wa Wi-fi ‘’ Jopo hilo linajumuishwa Yan Michalevsky, Dan Boneh na Aaron Schulman kutoka idara ya sayansi ya tarakilishi ka

MAFANIKIO; ukihitaji ufanikiwe fanya haya

Wakati huu ambao kila mtu anapambana nahali yake, ujasiriamali umekua kimbilio la vijana wengi, kama tunavyojua hakuna mtu anaeanzisha kitu kwa lengo la kufeli , japo sio wote hufanikiwa. Leo nawaletea sifa 4 za wajasiriamali waliofanikiwa na pengine ukiziiga, unaweza kuongeza nafasi ya kufanikiwa katika mishe zako. 1. PENDELEA KUAMKA MAPEMA Huwezi fanikisha malengo yako kama wewe ni mtumwa wa usingizi. siku zote pendelea kuamka mapema ili uweze kukamilisha kazi zilizobaki au ngumu ambazo unatakiwa uzikamilishe kwa siku husika maana  akili yako inakuwa bado ina nguvu ya kufanya mambo mengi na kwa ufanisi wakati wa asubuhi. mabilionea wengi duniani ikiwemo Mo Dewji, Bakhlesa, Dangote n.k. wana tabia ya kuamka mapema 2. PANGA SIKU YAKO MAPEMA  Ni vizuri kupangilia siku yako mapema ili kujua uamkapo utaanza na nini. Hii husaidia kazi zako kufanyika kwa mpangilio na kuokoa muda ambao utaruhusu akili yako kufanya kazi na kuvumbua vitu vya nyongeza. Pia itapelekea kuboresha bi

HEBU SOMA HII KWA MAKINI ITAKUSAIDIA SANA NA ITAKUGUSA TU

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, bali UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI... ✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. 👉🏾Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa wengi wao ni wale wa elimu ya chini kabisa, "darasa la saba” ama wale ambao hawakuingia darasani kabisa... 🙇🏽📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 🚙magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!) 👉🏾Wapo 🙇🏽📚wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.. 👉🏾Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayow

West Brom yamtimua kocha wake

West Brom imechukua maamuzi ya kumfuta kazi meneja Tony Pulis baada ya miaka mitatu akiwajibika, kufuatia klabu yake kupokea kichapo cha 4-0 dhidi ya Chelsea siku ya Jumamosi. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 anaacha jukumu lake kwa kuwa alishinda mara mbili tu katika michezo 21 ya mwisho ya ligi.. West Brom hawaja shinda katika ligi tangu Agosti 19 na Pulis kachana na  klabu hiyo baada ya karibu miaka mitatu akiwa na jukumu la ukocha, Mwenyekiti John Williams alisema: "Maamuzi haya hayakufikiwa hayapendezi hata kidogo lakini daima kwa maslahi ya klabu hiyo. "Sisi ni katika biashara ya matokeo ya juu ya mwisho  wa msimu uliopita na msimu huu hadi sasa, hali yetu imekuwa yakukatisha tamaa sana. "Tungependa kuweka kumbukumbu kwenye shukrani yetu ya mchango wa Tony na kazi ngumu wakati wa mpito kwa klabu hiyo ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya umiliki. Tunampenda tunamtakia kila la kheli katika juhudi zake za baadaye."