
Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo
ameitaka klabu ya Real Madrid kuweka bei yao ya kumuuza isiopungua
£89m). Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Ureno yuko tayari
kuondoka Uhispania.(Daily Record)
Mshambuliaji wa Chelsea Eden
Hazard, 26, hajakaataa kuongeza kandarasi na mabingwa hao watetezi wa
Uingereza licha ya madai kutoka kwa babake kwamba anataka kuhamia Real
Madrid.(Independent)
Wachezaji kadhaa wa Arsenal walidaiwa kumshutumu mshambuliaji Alexi Sanchez kwa kuwa na tabia mbaya baada ya mechi dhidi ya Burnley mwezi Novemba. (Guardian)

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Everton na Uingereza Ross Barkley, 24. (Telegraph)
West Ham itawasilisha ombi la kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jonjo Shelvey, 25, huku David Moyes akijaribu kuimarisha safu yake ya kati.. (Daily Mirror)

Nahodha wa West Brom Jonny Evans analengwa na klabu ya ManCity.
Mkufunzi wa klabu hiyo Alan Pardew alikiri kwamba klabu hiyo ingependelea kumuuza beki wa Ireland kaskazini Evans ili kukusanya fedha za kununua mshambuliaji (Mirror)

Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge anapendelea uhamisho wa Southampton lakini anahofia United itazuia uhamisho wowote chini ya £25m. (Daily Mirror)
Hatahivyo Southampton inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Stoke ambayo inajiandaa kuongeza kiungo wa kati mwengine katika kikosi chake. (Mail)

Juventus iko tayari kuanzisha makubaliano ya kuweka kandarasi na kiungo wa kati wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 23. (Corriere dello Sport - in Italian)
Mkurugenzi wa Everton Steve Walsh amesafiri hadi mjini Istanbul Uturuki ili kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Besiktas Cenk Tosun, 26, kufuatia waiwasi kutoka kwa vilabu vyengine vya Uturuki vinavyomuwinda (Times - subscription required)
Post a Comment