Skip to main content

Posts

VIDEO; alikiba amzungumzia baraka da prince

Alikiba - Seduce Me (Official Music Video)

TETESI ZA USAJILI ULAYA MAHREZ KWENDA MAN U

Bado masaa yasiyozidi 40 ili dirisha la usajili barani Ulaya kufungwa, kila timu inajaribu kupata sahihi ya mtu sahihi kwa ajili ya msimu huu wa ligi na matumizi makubwa ya pesa yanafanya muda huu uliobaki kuwa wa kuvutia. Thomas Lemar ambaye alikuwa anatajwa kuelekea Anfield kukipiga na klabu ya Liverpool inaonekana Barca wameingilia kati usajili huo na sasa wanataka kumnunua Lemar, taarifa zinadai Barca wanapambana kuipiku Liverpool ndani ya usiku wa leo au kesho. Oxlade Chamberlain naye amekuwa akizungumziwa sana hii leo, Chamberlain alikuwa akihusishwa kuelekea Stamford Bridge na inasemekana Chelsea walishakubali kutoa £35m ili kumnunua lakini leo habari mpya zinadai Chamberlain amekataa kujiunga na Chelsea na anataka aende Liverpool. Angel Di Maria anaweza kurudi tena katika ligi kuu ya Hispania La Liga, lakini kubwa zaidi ni kwamba safari hii Di Maria anarudi Hispania ambako anatakwa na wapinzani wakubwa wa timu yake ya zamani Real Madrid ambao ni Barcelona, taarif

Maneno ya alikiba baada ya kutajwa kama vijana 100 wa afrika wenye ushawishi

Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Alikiba kutajwa kuingia katika orodha ya vijana 100 wenye ushawishi Afrika 2017, ameelezea furaha yake. “Najisikia vizuri kwamba Africa nzima imekutambua, kuna watu ambao wanatamani kuwa kama Alikiba na vitu kama hivyo. Kwa hivyo nawahamasisha vijana wengine kufanya kazi nzuri kama mimi nivyofanya, nashukuru sana, najisikia vizuri,” ameiambia The Playlist ya Times Fm. Vijana wengine wa kitanzania waliotajwa katika orodha hiyo iliyotolewa na African Youth Awards  ni pamoja na Nancy Sumari, Diamond Platnumz, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Flaviana Matata, Millard Ayo na Jokate.

Lipumba ampigia magoti Maalim Seif amtaka arudi wayamalize ila kwa kumsikiliza mwenyekiti

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti. Profesa Lipumba amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya ofisi za Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo Buguruni, Lipumba amemtaka Katibu Mkuu huyo kurudi wafanye mazungumzo na atambue kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa CUF na ndiye boss wake. "Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze"

Bomoa bomoa dar yaipitia nyumba ya mkapa

TAARIFA RASMI YA CHAMA CUF JUU YA KUTOKA MAHAKAMANI LEO TAREHE -15/8/2017:

1. SHAURI LA WABUNGE 8 WA CUF NAMBA 479/2017 MAHAKAMA KUU IMEPANGA KUTOA MAAMUZI YA MAOMBI YA ZUIO LA MUDA KESHO SAA 7:30 MCHANA.  2. WALINZI WA CUF WALIOSINGIZIWA KUWA NA SILAHA NA VIRIPURISHI WASHINDA KESI MAHAKAMA YA KISUTU. 3. ORODHA YA MASHAURI YALIYOPO MAHAKAMANI MWEZI AUGUST, 2017. Mbele ya Mheshimiwa Jaji LUGANO MWANDAMBO leo amesikiliza hoja za Mapingamizi ya awali (Preliminary Objection) yaliyowekwa na Lipumba na wenzake na Attorney General-AG katika shauri la Madai namba 479/2017 dhidi ya Lipumba na wenzake 14 akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi NEC, na Katibu wa Bunge, upande wa Wabunge [8] na madiwani [2] umewakilishwa na Wakili Msomi Peter Kibatara. Maombi hayo yaliyofunguliwa Tarehe 4 August 2017 na kupangwa kusikilizwa leo Tarehe 15 August, 2017. Msingi wa mapingamizi hayo ni mrejeo wa yaleyale ya awali ambapo walidai kuwa Mahakama haina mamlaka ya kutoa Amri ya Zuio kwa Bunge na kwamba vifungu vilivyonukulwa na kuwekwa katika maombi hayo si sahihi.