Skip to main content

Posts

Pata matangazo kwa ajili ya blog yako

Hii ni kampuni inayokuwezesha kutangaza ads kwenye blog yako na pia kwa maadvertiser wana uwezo wa kuingia mkataba nao na kuanza kutangaza biashara zao mbalimbali. Kama bado mmiliki wa blog ujajiunga bado ujachelewa jiunge sasa na ufurahie malipo mazuri kutoka kwenye hii kampuni. Inalipa kutokana na impression na clicks kwenye ads ambazo zitakuwa kwenye blog yako. Kujiunga ingia seebait.com na ufuate maelekezo kama ifuatavyo 1.ingia seebait.com 2. scroll down hadi ukiona publisher 3. shuka chini hadi utakapoona signup/login here 4.click hapo 5.itakuletea option za kusign up sign up kwa kutumia gmail account yako na ufuate maelekezo ya kujiunga 6. kwa advertiser shuka chini hadi utakpoona neno advertise baada ya kufungua seebait.com hapo utajiunga na kufurahia huduma nzuri za matangazo KUMBUKA WEBSITE HII INA MASHARTI NA VIGEZO VYAKE INGIA HAPA KABLA NHUJAJIUNGA https://seebait.com/publisher/terms-and-conditions KAMA UNA SWALI COMMENT CHINI

Watuhumiwa ujambazi kibiti wauwawa

Katika eneo la utende kata ya Ikwiriri, Tarafa ya ya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji kanda Maalum ya Polisi Mkoa wa Rufiji, Askari Polisi walifanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea Wilaya tatu za kanda Maalumu ya Mkoa wa Kipolisi Rufiji. DCP Liberatus Sabaas amesema, Polisi imemuuwa kiongozi wa mauaji ya kibiti  Abdallah Ally Ngande Makeo aliyekuwa akitafutwa kipindi kirefu. Nafikiri hapa DCP Liberatus Sabaas amechanganya Majina kwani aliyekuwa anatafutwa Kipindi kirefu na Majina yapo kwenye magazeti anaitwa  Abdurshakur Ngande Makeo . Aidha atakuwa ni Mpya au majina amejichanganya. Majambazi walikuwa watano, askari wajibu mapigo na kuwajeruhi watu wawili kati ya wale watano ambao wamefariki wakati wakikimbizwa Hospitali ya Muhimbili. Katika tukio hilo, Polisi walikamata Silaha moja aina ya Rifle 375 ambayo imekatwa kitako na mtutu ikiwa na Risasi Mbili.

Tundu lissu akamatwa na polisi sababu hizi hapa

Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amekamatwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere International (JNIA) akielekea Kigali Rwanda kuhudhuria kikao cha Halmashauri ya EALS kinachotarajia kuanza hapo kesho. Kamanda wa Polisi wa Viwanda vya Ndege, Martin Ortieno amesema kuwa ni kweli Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS amekamatwa na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi. Aidha, Kamanda huyo wa viwanja vya Ndege Tanzania hakutaka kueleza sababu ambazo zimesababisha kukamatwa kwa Lissu hali ambayo imemsababishia kuahirishwa kwa safari yake ya Kigali. Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii huku sababu za kukamatwa kwake hazijawekwa bayana. “Lissu amekamatwa na watu ambao walijitambulisha kuwa ni maofisa Polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam lakini hawakuweza kumueleza kosa lake ni lipi hivyo wakaondoka nae kutoka u

ADC wamnasa Lissu, wasema hana uzalendo

Chama cha Alliance for Democratic Change, (ADC) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) kuomba msamaha kufuatia matamshi ya Mwanasheria wake Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu aliyoyatoa siku za hivi karibuni. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan Doyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  mapema hii leo jijiini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa matamshi hayo hayavumiliki kwa Mtanzania yeyote kusikia mwanasiasa mmoja akitaka kwenda kuishtaki nchi umoja wa mataifa ili isipate misaada. Amesema kuwa kama Chadema wameshindwa kushindana kisiasa ni bora wakawaeleza wafuasi wao kuwa hawawezi kushindana na Chama Cha Mapinduzi CCM lakini si kuanza kuichongea nchi kimataifa. “Hii ni nchi yetu sote, kamwe ugomvi wa ndani huwezi ukaupeleka nje hata siku moja, kwa hili wanalotaka kulifanya Chadema si jambo la kizalendo hata kidogo, wanataka kutuharibia nchi yetu, kama wameshindwa ni bora wakae pembeni,” amesema Doyo.

Vanessa afunguka kuhusu mapenzi yake na jux

Vanessa amefunguka na kusema bado anampenda na ataendelea kumpenda aliyekuwa mpenzii wake Jux ambaye hivi karibuni wameweka wazi kuvunjika kwa mahusiano yao. Pia ameeleza kuwa wimbo wa kisela ni wimbo ambao asilimia kubwa ni ukweli mtupu kuhusu  maisha halisi ya kimapenzi kati yake na aliyekuwa mpenzi wake Jux. ”Everything ambacho kimeandikwa kwenye kisela ni ukweli mtupu, unajua kuna tabia za kisela lakini mapenzi sio ya kisela” amesema Vanessa. Cash madam ameeleza kuwa  alirekodi wimbo wa Kisela akiwa analia kutokana huzuni kubwa aliyokuwa nayo moyoni kipindi hicho. Na amefunguka kuwa mapenzi yake na Jux yalivunjika miezi mitano iliyopita, japo hivi karibuni wawili hao wamefunguka hadharani kuhusu kuvunjika kwa penzi lao. Kupitia mahojiano yaliyofanyika Vanessa hakutaka kufunguka chanzo cha mapenzi yake na Jux kuvunjika akidai kuwa wapo vizuri na wanaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali. Na hilo linadhibitishwa pindi ambapo Jux alihitimu masomo yake Vanessa Md

JPM: Acha niwanyooshe ndipo nisafiri

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, John Pombe Magufuli amesema kwa sasa hatoweza kusafiri kwenda nchi yeyote, ataendelea kumtumia muwakilishi wake ili yeye abaki kuinyoosha nchi na kuwashughulikia Watanzania wajanja. Amesema hadi sasa amepata mialiko 60 kutoka nchi za nje mbalimbali, lakini hatokwenda. Ameeleza kuwa alitakiwa kusafiri kwenda Ethiopia kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU), lakini ameona amtume Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ili amuwakilishe ili yeye aendelee na majukumu mengine ya nchi. Magufuli amewaomba Watanzania wenye nia njema na nchi yao wamuombee ili ashughulikie changamoto za nchi hii kwani anawasiwasi anaweza kumaliza kipindi chake cha uongozi na mambo yakabaki hivyohivyo. ”Ndiyo maana sitembei sana, nimeshapata mialiko 60, siendi, nikienda huko watafanya ajabu ngoja nideal nao kwanza’ amesema Magufuli. Magufuli alitoa kauli hizo jana mjini Sengerema katika ziara yake ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Nyamazugo, mkoani Mw

Tumia simu yako kutokomeza wizi tambua kitu chako kilipo

Wataalam wa teknolojia wamegundua njia ambayo inaweza kuwa mwarubaini wa watu kutopoteza vitu vyao kirahisi kwa kuvibaini popote vilipo kwa kutumia simu za kisasa (Smartphone). Teknolojia mpya iliyopewa jina la  TrackR  itawasaidia zaidi watu wengi waliokuwa wanashindwa kujiunga na huduma mbalimbali za kuwekea ulinzi vyombo vyao vya usafiri (track) ili kubaini vilipo, kwa kuzingatia kuwa mtu huhitaji kulipia gharama za kila mwezi kwa huduma hiyo inayotolewa na makampuni mbalimbali yanayotumia mfumo wa ‘GPS’. Kampuni moja imebuni kifaa kinachofahamika kama Track R kinachouzwa kwa bei ambayo watu wengi wenye uchumi wa chini wanaweza kununua, kinachounganishwa na simu ya kisasa ya mtumiaji husika. Mtumiaji anapaswa kufunga kifaa hicho kidogo kwenye kitu anachotaka, kisha ata-download application ya ‘Track R’ kwenye simu yake ya mkononi ya (iPhone au Smartphone) na kuiunganisha na kifaa hicho. Baada ya kukamilisha utaratibu huo, simu yake itakuwa na uwezo wa kumueleza mahali popo