Ticker

6/recent/ticker-posts

Vanessa afunguka kuhusu mapenzi yake na jux

Vanessa amefunguka na kusema bado anampenda na ataendelea kumpenda aliyekuwa mpenzii wake Jux ambaye hivi karibuni wameweka wazi kuvunjika kwa mahusiano yao.
Pia ameeleza kuwa wimbo wa kisela ni wimbo ambao asilimia kubwa ni ukweli mtupu kuhusu  maisha halisi ya kimapenzi kati yake na aliyekuwa mpenzi wake Jux.
”Everything ambacho kimeandikwa kwenye kisela ni ukweli mtupu, unajua kuna tabia za kisela lakini mapenzi sio ya kisela” amesema Vanessa.
Cash madam ameeleza kuwa  alirekodi wimbo wa Kisela akiwa analia kutokana huzuni kubwa aliyokuwa nayo moyoni kipindi hicho.
Image result for vanessa jux
Na amefunguka kuwa mapenzi yake na Jux yalivunjika miezi mitano iliyopita, japo hivi karibuni wawili hao wamefunguka hadharani kuhusu kuvunjika kwa penzi lao.
Kupitia mahojiano yaliyofanyika Vanessa hakutaka kufunguka chanzo cha mapenzi yake na Jux kuvunjika akidai kuwa wapo vizuri na wanaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali.
Na hilo linadhibitishwa pindi ambapo Jux alihitimu masomo yake Vanessa Mdee alimpost kwa kumpa hongera na Jux nae alipost kuonesha kuwa anatambua mchango mkubwa wa Vanessa katika kuhitimu masomo yake.
Na hayo yote yalitokea kipindi ambacho wawili hao tayari wamekwishatengana kimapenzi.
Aidha Vanessa ameeleza kuwa hatakuwa tayari tena kuweka mahusiano yake ya kimapenzi hadharani kama ilivyokuwa yeye na Jux.

Post a Comment

0 Comments