Ticker

6/recent/ticker-posts

Watuhumiwa ujambazi kibiti wauwawa


Katika eneo la utende kata ya Ikwiriri, Tarafa ya ya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji kanda Maalum ya Polisi Mkoa wa Rufiji, Askari Polisi walifanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea Wilaya tatu za kanda Maalumu ya Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

DCP Liberatus Sabaas amesema, Polisi imemuuwa kiongozi wa mauaji ya kibiti Abdallah Ally Ngande Makeoaliyekuwa akitafutwa kipindi kirefu. Nafikiri hapa DCP Liberatus Sabaas amechanganya Majina kwani aliyekuwa anatafutwa Kipindi kirefu na Majina yapo kwenye magazeti anaitwa Abdurshakur Ngande Makeo. Aidha atakuwa ni Mpya au majina amejichanganya.

Majambazi walikuwa watano, askari wajibu mapigo na kuwajeruhi watu wawili kati ya wale watano ambao wamefariki wakati wakikimbizwa Hospitali ya Muhimbili. Katika tukio hilo, Polisi walikamata Silaha moja aina ya Rifle 375 ambayo imekatwa kitako na mtutu ikiwa na Risasi Mbili.


Post a Comment

0 Comments