Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2017

MAFANIKIO; ukihitaji ufanikiwe fanya haya

Wakati huu ambao kila mtu anapambana nahali yake, ujasiriamali umekua kimbilio la vijana wengi, kama tunavyojua hakuna mtu anaeanzisha kitu kwa lengo la kufeli , japo sio wote hufanikiwa. Leo nawaletea sifa 4 za wajasiriamali waliofanikiwa na pengine ukiziiga, unaweza kuongeza nafasi ya kufanikiwa katika mishe zako. 1. PENDELEA KUAMKA MAPEMA Huwezi fanikisha malengo yako kama wewe ni mtumwa wa usingizi. siku zote pendelea kuamka mapema ili uweze kukamilisha kazi zilizobaki au ngumu ambazo unatakiwa uzikamilishe kwa siku husika maana  akili yako inakuwa bado ina nguvu ya kufanya mambo mengi na kwa ufanisi wakati wa asubuhi. mabilionea wengi duniani ikiwemo Mo Dewji, Bakhlesa, Dangote n.k. wana tabia ya kuamka mapema 2. PANGA SIKU YAKO MAPEMA  Ni vizuri kupangilia siku yako mapema ili kujua uamkapo utaanza na nini. Hii husaidia kazi zako kufanyika kwa mpangilio na kuokoa muda ambao utaruhusu akili yako kufanya kazi na kuvumbua vitu vya nyongeza. Pia itapelekea kuboresha bi

HEBU SOMA HII KWA MAKINI ITAKUSAIDIA SANA NA ITAKUGUSA TU

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, bali UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI... ✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. 👉🏾Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa wengi wao ni wale wa elimu ya chini kabisa, "darasa la saba” ama wale ambao hawakuingia darasani kabisa... 🙇🏽📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 🚙magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!) 👉🏾Wapo 🙇🏽📚wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.. 👉🏾Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayow

West Brom yamtimua kocha wake

West Brom imechukua maamuzi ya kumfuta kazi meneja Tony Pulis baada ya miaka mitatu akiwajibika, kufuatia klabu yake kupokea kichapo cha 4-0 dhidi ya Chelsea siku ya Jumamosi. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 anaacha jukumu lake kwa kuwa alishinda mara mbili tu katika michezo 21 ya mwisho ya ligi.. West Brom hawaja shinda katika ligi tangu Agosti 19 na Pulis kachana na  klabu hiyo baada ya karibu miaka mitatu akiwa na jukumu la ukocha, Mwenyekiti John Williams alisema: "Maamuzi haya hayakufikiwa hayapendezi hata kidogo lakini daima kwa maslahi ya klabu hiyo. "Sisi ni katika biashara ya matokeo ya juu ya mwisho  wa msimu uliopita na msimu huu hadi sasa, hali yetu imekuwa yakukatisha tamaa sana. "Tungependa kuweka kumbukumbu kwenye shukrani yetu ya mchango wa Tony na kazi ngumu wakati wa mpito kwa klabu hiyo ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya umiliki. Tunampenda tunamtakia kila la kheli katika juhudi zake za baadaye."

MUGABE APEWA SIKU KUACHIA MADARAKA, VIONGOZI WAJIPANGA KUMFUNGULIA MASHTAKA YA UHALIFU

Waziri wa chama c cha Zanu-PF cha Zimbabwe wanajitayarisha kukutana na kujadili uhalifu wa Rais Robert Mugabe, baada ya mwisho wa kujiuzulu kwake na kuja Jumatatu. Siku ya mwisho iliwekwa na chama cha Mugabe mwenyewe, Zanu-PF. Kiongozi huyo alisisitiza wananchi wa Zimbabwe siku ya Jumapili, akitangaza kwenye TV kwamba alipanga kubaki kama rais. Zanu-PF inasema kuwa ni nyuma ya uhalifu, na kesi zinaweza kuanza mapema Jumanne wakati bunge litakutana. Ushiki wa Mugabe juu ya nguvu umepungua sana tangu jeshi la nchi liliingilia Jumatano mfululizo juu ya nani atakayefanikiwa. Mgogoro huu ulianza wiki mbili zilizopita wakati kiongozi mwenye umri wa miaka 93 alipomfuta kazi naibu wake Emmerson Mnangagwa, makamanda wa jeshi  waliiona kama ni jaribio la kumuweka mke wake Grace kama Rais wa pili. Zimbabwe tangu wakati huo imekua na mikutano mikubwa ya barabara inayoshinikiza  kujiuzulu kwa Mugabe mara moja. Maandamano hayo yamesaidiwa na wapiganaji wa Vita walioathiriwa - ambao walipi

CONTE MBIONI KUTIMKA CHELSEA

Rais wa Shirikisho la Soka la Carlo Carlo Tavecchio amethibitisha kuwa bosi wa Chelsea Antonio Conte atakuwa chaguo lake la kwanza kuwa mkufunzi mpya wa Azzurri. Conte aliacha kazi ya Chelsea baada ya Euro 2016, lakini nafasi ya Giampiero Ventura imechukuliwa baada ya Italia kupoteza mchezo wao kati Sweden katika mchezo wa Kombe la Dunia. Mchungaji wa Juventus Allegri amesema anataka kuwa bosi wa Italia siku moja lakini "si wakati huu" na wakati meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini ni bosi wa Zenit St Petersburg, Carlo Ancelotti inapatikana baada ya kufungwa na Bayern Munich. Mchezaji wa zamani wa Juventus Conte aliongoza Chelsea kwenye cheo cha Ligi Kuu baada ya kuondoka Italia, ambaye aliongoza kwa robo fainali ya Euro 2016. Hata hivyo kuna ripoti ya mara kwa mara kwamba yeye hafurahi katika Stamford Bridge. Tavecchio alimshtaki kocha wa zamani wa Torino Ventura kwa kushindwa kwa Azzurri kufikia Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1958. &qu

WACHINA WATIWA MBALONI DAR ES SALAAM

Raia wanne wa China wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuendesha kiwanda cha kutengeneza mifuko ikiwemo ya plastiki kinyume na sheria huku kiwanda hicho kikitozwa faina ya shilingi Milioni 7 kwa makosa ya kisheria. Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakati wa ziara yake jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa raia hao wa kigeni wamekiuka taratibu na sheria za uendeshaji kiwanda kilichopo kwenye makazi ya watu na kuagiza kifungwe kwa muda ili kupisha uchunguzi wa usajili wake. Amesema serikali inawapenda wawekezaji kwenye sekta ya viwanda na inataka waje kwa wingi kuwekeza nchini lakini ni lazima nao wafuate sheria za nchi katika uwekezaji wao ili kila upande uweze kufaidika na uwekezaji huo.

DKT LOUS SHIKA TAYARI KUTUMIWA MABILION YAKE KUTOKA URUSI

Dkt. Louis Shika ambaye alijizolea umaarufu baada ya kutangaza dau kununua nyumba tatu za mfanyabiashara Said Lugumi kwa shilingi bilioni 3.2 zilizokuwa zikipigwa mnada na kampuni ya Yono lakini akashindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo, ameanza mchakato wa kurejesha fedha zake zilizopo nje ya nchi. Amesema kuwa leo jumamosi amelipa Dola 100 za Kimarekani sawa na shilingi (220,000) za Kitanzania kwa ajili ya bima ili aweze kutumiwa fedha zake nchini. Dkt. Shika amesema hayo mara baada ya kukutana na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alipokuwa ametembelea Shirika la Posta kuzungumza na wafanyakazi, walimkuta Dkt. Shika akiwa katika shirika hilo, na kudai kuwa yupo hapo kwa ajili ya malipo. “Nimelipa dola 100 za bima ili kukamilisha fedha zangu zije na nilipie zile nyumba, hili la bima lilikuwa ni muhimu sana kwangu,”amesema Dkt. Shika Hata hivyo, nyumba moja ilishauzwa kwa mhindi aliyeshika namba mbili

KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS CHATAJWA

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Ammy Ninje ametaja majina 20 ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu hiyo itakayoshiriki michuano ya CECAFA Challenge mwaka huu. Kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 27 mwaka huu kujiandaa na michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu nchini Kenya. Aidha, kikosi hicho kinaundwa na makipa, Aishi Manula na Peter Manyika,wakati walinzi ni Boniphace Maganga, Gadiel Michael, Kevin Yondan na Erasto Nyoni. Wengine ni Mohamed Husein na Kennedy Wilson. Viungo ni Himid Mao, Hamis Abdallah, Mzamiru Yassin na Rafael Daudi. Wengine ni Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib na Abdul Hilal, huku washambuliaji ni Elias Maguli, Mbaraka Yusuph, Yohana Mkomola na Daniel Lyanga.

TETESI ZA USAJILI KATIKA MAGAZETI YA UINGEREZA LUIZ TO MAN U

Daily Express.  Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anatajwa kuwa mbionj kujaribu kumshawishi David Luiz ajiunge naye ifikapo mwezi wa kwanza baada ya beki huyo kutajwa kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha wa Chelsea. Daily Mirror. Klabu ya Liverpool sasa italazimika kutoa kiasi cha £70m kwa ajili ya kumnunua mliniz wa Southampton Virgil Van Djik ambaye wamekuwa wakimtaka kwa muda mrefu na sasa kocha wa Southampton amesema wako tayari kumuachia kama wakipata kiasi hicho. Daily Star. Steve Kaplan ambaye ni moja kati ya wamiliki wa klabu ya Swansea amepiga kura ya kutokuwa na imani na kocha wa Swansea Paul Clement na sasa kocha huyo anakuwa amekalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo. The Sun. Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal na pia Manchester City Emmanuel Adebayor ameishutumu familia yake kwamba ilimfanya atamani kujiua zaidi ya mara tatu kutokana na matatizo yaliyosababishwa na familia hiyo. Daily Mail. Klabu ya soka ya Manchester United imezipiga chini tete