Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2017

RC Makonda akabidhiwa ripoti ya wezi wa vifaa vya magari Dar, 73 mbaroni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa ripoti ya wezi wa magari pamoja na vifaa vya magari na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Lucas Mondya ikiwa ni miezi kadhaa toka mkuu huyo aliagize jeshi hilo baada ya matukio ya namna hiyo kushamiri ndani ya mkoa huo. RC Makonda akionyeshwa na DCP, Mkondya baadhi ya vifaa vya magari vilivyokamatwa. Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi hii wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lucas Mondya alisema katika opesheni hiyo kali jumla ya wahumiwa 73 wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, power windows, radio, injector pump, starter na seat cover. “Tarehe 19 mwezi wa saba mweshimiwa RC Makonda ulitoa maagizo kwa jeshi la polisi kwamba unatupatia siku saba kuhakikisha tunasambaratisha mtandao wa wezi wa vifaa vya magari pamoja na magari baada na sisi tumelitekeleza hilo tayari kuna watu 73

Neymar ataka kuzichapa uwanjani atupa jezi ya barcelona mazoezini

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar Dos Santos leo ametawala upya vichwa vya habari  baada ya kuvua jezi ya mazoezi ya Barcelona na kuondoka uwanjani. Neymar alikuwa mazoezini na katika hali ya kawaida kulitokea kutokuelewana kati yake na mchezaji mpya wa klabu hiyo Nelson Semedo ndipo Neymar alipokasirika. Neymar alionekana kutaka kumkabili Semedo lakini wakati anamfuata huku akionekana mwenye hasira ndipo Sergio Bosquet na Javier Mascherano walimzuia. Baada ya Neymar kuzuiwa kuendeleza ugomvi alivua jezi maalumu ya mazoezi (bibs) akaitupa pembeni kisha akaupiga mpira kwa hasira na kuondoka zake. Neymar amefanya tukio hilo katika kipindi hiki ambacho anahusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu ya PSG na huku ikitajwa kwamba hana furaha na Barcelona. Tukio hili limezidi kuongeza tetesi kwamba Neymar anaweza kuondoka Barca lakini Barca kwa upande wao pia wamechoshwa  na tabia za Neymar haswa starehe zake.

Real madrid kuvunja record ya dunia

Baada ya vilabu vingi kuhusishwa kumsajili mchezaji chipukizi wa Monaco, Kylian Mbappe, hatimaye klabu ya Real Madrid imetangaza kufikia makubaliano na Monaco kumsajili mchezaji huo. Madrid imetangaza kuwa itamsajili Mbappe kwa pauni milioni 161 ambazo kwa pesa ya kibongo inafikia bilioni 360, uhamisho ambao utavunja rekodi ya dunia ya usajili iliyokuwa ikishikwa na Paul Pogba aliyesajiliwa na Man United kutoka Juventus kwa pauni milioni 89. Mbappe mwenye umri wa miaka 18 tayari amekuwa na kiwango kikubwa cha soka ambacho kinazivutia klabu nyingi barani Ulaya iwapo uhamisho huo utafanyika kama umevyotangazwa basi atasaini mkataba wa miaka sita. Uamuzi wa Real Madrid kumsajili Mbappe umekuja ikiwa ni siku kadhaa kupita baada ya kumuuza mshambuliaji wake Alvaro Morata kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, Chelsea na kumtoa kwa mkopo kiungo James Rodriguez kwa mkopo kwenda Bayern Munich ya Ujerumani. credit http://dewjiblog.co.tz/

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULY 25,2017

Fifa yampa kifungo Bailly

Shirikisho la soka barani Ulaya ‘UEFA’limemfungia beki wa Manchester United Eric Bailly   kucheza michezo mitatu kutokana na kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Europa League dhidi ya Celta Vigo. Bailly alitolewa nje katika mchezo wa pili wa Europa League katika sale ya 1-1 dhidi ya Celta Vigo uliopigwa katika dimba la Old Trafford na alikosa mchezo wa fainali dhidi ya Ajax. Mchezaji huyo alonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na ugomvi na mshambuliaji wa Celta Vigo John Guidetti katika mchezo Kamati ya nidhamu ya UEFA imemuongezea adhabu EricBailly kwa kumfungia kukosa michezo mitatu hii ikimaanisha kwamba ataukosa mchezo wa fainali ya Super Cup dhidi ya Real Madrid. Eric Bailly katika ugonvi na mchezaji wa Celta Vigo Man United imefuzu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na kwa adhabu aliyoipata  beki huyo raia wa Ivory Coast atakosa pia mchezo wa ufunguzi wa michuno hiyo.

Simulizi ya mapenzi

Nilikua mwajiriwa katika kampuni moja maarufu jijini dare s salaam , katika kuajiriwa kwangu huko nikawa msaidizi maalumu wa bosi wa kampuni ile , basi siku moja moja nilikuwa naenda kujirusha na bosi wangu .   Ukizingatia kwamba sikuwa na mume wala mchumba na kwa kweli huyu bosi ndio alikuwa mtu wa kwanza kufanya nae tendo la ndoa , hivyo nilifurahia mhemko wake na jinsi alivyokuwa ananipenda na kunijali kila kitu nilipata na zaidi . Alifanya yote haya bila kunificha kwamba ana mke na watoto nyumbani kwake kwahiyo wakati mwingine chochote kinaweza kutokea nijiandae kwa shuguli hiyo pevu kama mke wake akishitukia dili hilo . Tulikuwa na uhusiano na huyu bosi kwa miezi 4 hivi mpaka siku moja katika tembea tembea mitaani nikakutana na kijana mmoja mtanashati akanieleza kwamba ananipenda na kunizimia sana yaani ameshanifia Huyu kijana alihangaika kwa mwezi mzima mpaka siku nikaja kumkubalia akawa ndio mpenzii wangu halali sasa , nilimwamini sana nay eye aliniamini sana , miezi 3 t

RAIS Magufuli Afunguka...Siogopi Kufungwa.......

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ‘JPM’ amesema yeye kama kiongozi mkuu wa nchi haogopi vitisho vya kufungwa ama kushtakiwa vinavyotajwa na baadhi ya wanasiasa baada ya kuwashughulikia wawekezaji wanaokiuka mikataba na kuhujumu uchumi wa nchi na badala yake ataendelea kuwatetea Watanzania wanyonge ili wapate haki yao. JPM ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini humo. “Hii nchi imejaa mafisadi, wamo wa CCM, Chadema, CUF, ACT, wazungu na wengine hawana chama. “Siogopi kufungwa, kama mliniteua niwatetee, nitawatetea kwa nguvu zangu zote juu ya majizi, tumeibiwa vya kutosha, madini yetu yanachimbwa yanapelekwa nje na hatupati kitu. “Wengine wamelipwa pesa ili kupinga tusichukue hatua dhidi ya majizi, nawaambia mimi kama rais nimejitoa kufa na kupona mpaka nihakikishe mali za Watanzania wanyonge haziibiwi na haki yao wanaipata. “Watambue kwamba sitafungwa badala yao majizi ndiyo yatafungwa. Ilikuwa lazima tubadilishe sheria zetu hatuwe

NYAMA ya Kitimoto Chamharibu Wema Sepetu.

Siku chache baada ya kubainika kuwa, Miss Tanzania 2006-07 ambaye pia anatisha katika tasnia ya filamu nchini, Wema Isaak Sepetu ni mtumiaji mzuri wa nyama ya Nguruwe ‘Kitimoto’, imeonekana kuwa msosi huo umeanza kumharibu kwa kutokwa na minyama uzembe. Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, kwasasa mrembo huyo ameongozeka unene na kuwa na ‘shavu dodo’ tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma kidogo, huku utumiaji wa nyama hiyo ukitajwa kama chanzo. Akiongea na Mwandishi Wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, ulaji wa Kitimoto kwa Wema huenda ukamuathiri kwani kwa muda mfupi ‘figa’ yake imeanza kubadilika. “Yaani Wema kwa Kitimoto usimpimie kabisa, lakini sasa ulaji wa nyama hiyo umeanza kuuharibu mwili wake kwani katoka minyama uzembe, nimekuwa nikimshauri ale kwa kiasi lakini mwenyewe anaona sio ishu,”alisema shoga huyo wa karibu na Wema. Katika siku za hivi karibuni, Wema alinaswa akipata nyama ya Kitimoto pamoja na ndizi za kuchoma katika baa moja b

DOWNLOAD; nyimbo mpya ya alikiba #JOHOTENA

Download ommy dimpoz new song

Download

Genk vs Everton Samatta, Rooney watupia angalia magoli yote hapa

SIMULIZI YA KWELI YA KUSISIMUA NA KUSIKITISHA YA MTOTO JANETH :

Kengele ya kutoka darasani iligongwa, wanafunzi wa shule ya msingi wakaanza kutoka madarasani huku wakifukuzana wengine wakipiga kelele ilimradi shwangwe tu. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufundisha shule za hatua hiyo. Ilikuwa ni shule ya serikali. Jicho langu liliangukia katika sura ya msichana mdogo, nguo zake chafu. Alikuwa analia. Alikuwa peke yake na hakuwa na yeyote wa kumbembeleza. Mimi kama mwalimu sikutaka kujisogeza karibu naye sana. Kwanza nilikuwa mgeni. Nikaachana naye. Siku iliyofuata tukio kama lile likajirudia. Msichana yuleyule wakati ule uleule wa kutawanyika, alikuwa analia sana. Mwishowe aliondoka huku akiwa analia. “Mbona mwenzenu analia?” nilimuuliza mwanafunzi mmoja. “Huyo ni mama kulialia..” alinijibu huku anacheka. Haikuniingia akilini hata kidogo kuwa yule binti analia bila sababu. Siku ya tatu nikaanza kujiweka karibu naye. Muda wa mapumziko nilimwita nikamnunulia chai, alikuwa ananiogopa na hakutaka kuniangalia machoni. Sikumuuliza lolote juu ya tabia ya

SIMULIZI YA KOSA LANGU:

SIMULIZI YA KOSA LANGU:  AUTHOR : ADELA DALLY KAVISHE Joyce ni msichana aliyezaliwa katika familia ya watoto wawili akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mzee Ndesanjo, maisha yao yalikuwa ni maisha ya furaha na amani walikuwa wakiishi Mkoa wa Dar es salaam maeneo ya Kimara Stop Over, lakini furaha hiyo ilipotea baada ya siku moja ambapo Mzee Ndesanjo alikuja nyumbani baada ya kutoka kazini na moja kwa moja akimtaka mama Joyce ajiandae kwani wangesafiri siku hiyo ambapo ilikuwa ni siku ya jumanne mida ya saa kumi na mbili jioni.Mzee Ndesanjo alikuwa na gari aina Eskudo alifika na kuita kwa sauti "Mama Joyce Mama Joyce" huko chumbani mama Joyce alimskia na kuitika "Bee Mume wangu,vipi mbona unaonge kwa sauti sana si ungeingia ndani kwanza" alisema mamaJocye huku akiwa anamuangalia mume wake kwa makini Baba Joyce alimsogelea huku akisema "hakuna muda wa kupoteza mimi ndani siingii nenda kajiandae tunasafari ya kwenda Morogoro kuna matatizo kwani rafiki yang

Jinsi ya ku-track simu yako na kujua mahali ilipo

Upotevu wa simu yako ni moja ya jambo baya watu wanalipata.Unaweza kuibiwa simu yako iliyokuwa imehifadhi data nyingi binafsi. Kwa msaada jinsi ya kupata simu yako iliyopotea, Google na Apple kwa pamoja wana njia za kufuatilia hili kutafuta mfumo wa simu yako. Jinsi ya kutafuta iPhone iliyopotea Ufumbuzi wake upo kwenye Find My iPhone.Huduma hii ina uwezo wa kukuonyesha kifaa chako chochote cha iOS Kupata uwezo juu ya iPhone yako,fuata hatua hizi; 1.Nenda kwenye setting/mpangilio wa iPhone yako 2.Shuka chini utakuta iCloud 3.Katika chini ya orodha bonyeza "Find My iPhone" 4.Kwenye Find My Phone switch on position 5.Ukiwa hapo ni wazo zuri ku-turn on send last  location Baada ya kuwezesha Find My iPhone,unaweza kuifuatilia vizuri simu yako iliyopotea na kuibiwa Jinsi ya kupata Android phone Kwa android ni tofauti kidogo na Apple.Google wameweka app yao kwenye Play store  na unaweza ku-download 1.Search Play Store "Android Device Manager" 2.Inst

Tumia simu yako kama mounse ya komputa

New Trick Habari za wakati huu msomaji wa Blog yako pendwa ya  DODY BLOG ! Katika mfululizo wa makala za wiki hii, leo tutaangalia jinsi ya  KUTUMIA   simu yako hio ya  SmartPhone kama  Mouse  ya kompyuta. FAIDA >>>Hii inaweza kukusaidia pale ambapo hauna Mouse kwa ajili ya compyuta yako, au  TouchPad  ya Laptop yako haifanyi kazi! Yani  inasumbua! MAHITAJI >> Utahitajika kuinstall program na App ntakazokupa hapa chini! Unaweza kutumia Apps mbalimbali na step ni hizihizi.  Host file utaiinstall kwenye kompyuta yako na App utaiweka kwenye simu yako, halafu utaunga compyuta yako kwenye wireless ya simu yako au bluetooth!  (Lengo la kuunga ni kuweka mawasiliano kati ya simu na kompyuta). kwa hio unaweza kutumia  Bluetooth au Wireless!  Zote ni sawa ila hapa nitaelezea Wireless. HATUA KWA HATUA 1.   Download na install  Monect  kwenye simu yako  HAPA! Install Monect Portable 2. Kwenye PC yako download na install  Monect Host  kwa kuclik  HAPA