Shirikisho la soka barani Ulaya ‘UEFA’limemfungia beki wa Manchester United Eric Bailly kucheza michezo mitatu kutokana na kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Europa League dhidi ya Celta Vigo.
Bailly alitolewa nje katika mchezo wa pili wa Europa League katika sale ya 1-1 dhidi ya Celta Vigo uliopigwa katika dimba la Old Trafford na alikosa mchezo wa fainali dhidi ya Ajax.
Mchezaji huyo alonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na ugomvi na mshambuliaji wa Celta Vigo John Guidetti katika mchezo
Kamati ya nidhamu ya UEFA imemuongezea adhabu EricBailly kwa kumfungia kukosa michezo mitatu hii ikimaanisha kwamba ataukosa mchezo wa fainali ya Super Cup dhidi ya Real Madrid.
Man United imefuzu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na kwa adhabu aliyoipata beki huyo raia wa Ivory Coast atakosa pia mchezo wa ufunguzi wa michuno hiyo.
Post a Comment