Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2017

MOURINHO AWAPONDA WASHAMBULIAJI WAKE

Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amewalaumu washambuliaji wa yimu yake ya Manchester United katika mechi dhidi ya Anderlecht baada ya timu hiyo kusawazisha katika dakika za mwisho za mechi ya robo fainali ya kombe la Yuropa. United iliongoza 1-0 nchini Ubelgiji hadi dakika 86 wakati waandalizi wa mechi hiyo waliposawazisha ikiwa ni shambulio lao la kwanza. ''Iwapo ningekuwa mlinzi wa man united ningekasirishwa sana na washambuliaji,alisema Mourinho''. ''Mabeki walifanya kazi ya kutosha lakini washambuliaji wakashindwa kuamua matokeo ya mechi hiyo'',alisema Mourinho

Marekani yatumia bomu kubwa zaidi kushambulia IS

Jeshi la Marekani kwa mara ya kwanza limewashambulia wapiganaji wa kundi la Islamic State kwa kutumia bomu kubwa lisilokuwa la nyuklia, kuwahi kutumiwa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, katika vita. Bomu hilo aina ya GBU-43 ambalo limetumika kutekeleza shambulio hilo, kipimo chake cha nguvu kilichotumika kinalingana sawa na tani 11 za TNT, na ambalo pia hujulikana kama ''Mama wa mabomu yote'' lilipigwa katika mapango yanayotumiwa na wapiganaji wa Islamic State kujificha katika jimbo la Nangarhar, mashariki mwa Afghanistan. Akielezea kulipuliwa kwa bomu hilo ardhini Gavana katika Wilaya ya Achin jimboni humo, Esmail Shinwari amesema ni kama vile miale mikali ilimeza eneo hilo. Mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan, Jenerali John Nicholson amesema bomu hilo lilikuwa ni zana sahihi kutumika kuendeleza kasi ya kupambana na waislamu hao wenye itikadi kali. Akitoa taarifa Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer amesema tahadhari zilichukuliwa kupun

Rais Magufuli Kuzindua Mabweni Mapya Chuko Kikuu cha Dar es Salaam

MAJAMBAZI WALIO WAUA ASIKARI 8 NAO WAUAWA

Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku. Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao. Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao. Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi. Amewataja askari wa

RAIS MAGUFURI ASIKITISHWA NA MAUAJI YA ASKALI 8

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi. Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo. “Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao  wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu. “Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu”  amesema Mhe. Rais Mag

TCRA yazitoza faini kampuni za simu, Zadaiwa kutozingatia vigezo vya utoaji huduma

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya milioni 65 kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya  9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za 2011 Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alizitaja kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited Zantel, Mic Tanzania Limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications Company Limited, TTCL huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma bora. "TCRA inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini kuhakikisha mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali ya juu (Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano ya mwaka 2011".  Alisema Kilaba Aidha Mhandisi huyo alisema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshi

CCM YAPATA UGENI KUTOKA CHADEMA

.. Leo 09 April 2017 Viongozi wa CHADEMA wilayani Ilemela wa mehamia CCM...Katika Mkutano wake wa ndani akiwa Ziarani Mkoani Mwanza ambapo Viongozi hao wa Chadema, BAVICHA na BAWACHA wa Wilaya ya Ilemela wameelezea kuchoshwa kwao dhidi ya Ukiukwaji wa Demokrasia, Ufisadi na Dhuluma ndani ya CHADEMA. CHADEMA kimeendelea kukiuka misingi ya kidemokrasia ndani ya chama na hata ndani ya bunge. Mifano ya hivi karibuni tukumbushane tu Mbowe aliwapoka wanachama haki ya kugombea na kuchaguliwa ktk bunge la Afrika Mashariki na badala yake akaja na majina yake mawili mfukoni ( Wenje na Masha). Lakini pia mkoani Kilimanjaro Mbowe amevuraga mchakato wa kugombea uenyekiti wa CHADEMA ili ampe zawadi Mzee Ndesamburo "ndesapesa". Kanda ya Nyanza demokrasia ilinyongwa ambapo Peter Msigwa alipewa zawadi ya uenyekiti makamanda wakisalia kulalama wasiwe na la kufanya. Mifano ni mingi kwa leo imetosha. "CHADEMA KINAHUBIRI UNYWAJI WA MAJI HUKU MBOWE ANAKUNYWA MVINYO"

NAPE; WANAO NIITA SHUJAA WATANIGEUKA

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amedai wanaomuita shujaa leo ipo siku wanaweza kumgeuka kwa sababu kama binadamu bado ana safari ndefu na anaweza kujikwaa ndiyo maana hataki kulivaa jina hilo bali anahitaji watanzania waendelee kumuombea.                                                                                                                   Nape Nnauye Akizugumza akiwa Mtama Mh. Nnauye amesema hawezi livaa jina hilo  bali amelipokea kwakuwa wananchi wameamua kumpatia jina hilo kwani hata sababu za kuitwa jina hilo zipo tofauti tofauti. "Sikatai kuitwa Shujaa kwa sababu wao wenyewe ndiyo wameniita, lakini siyo jambo ambalo nitalivaa.  Hao hao wanaoniita shujaa siku nyingine wanaweza kunigeuka kwa sababu binadamu ukiwa hai unaweza kujikwaa safari bado ni ndefu nachotaka kuwaomba tu wananchi waendelee kuniombea. Hata hivyo sababu za kuitwa shujaa kila mtu ana sababu yake, mwingine atakuambia kwa sababu hujatetereka wengine wanasema um

BANDA SIMAMISHWA KUCHEZA LIGI KUU TANZANIA BARA

Beki wa Simba, Abdi Banda amesimamishwa kucheza Ligi Kuu wakati akisubiri suala lake la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla wakati akiwa hana mpira kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF Abdi Banda Banda anadaiwa kufanya kitendo hicho ambacho hakikuonwa na waamuzi katika mechi kati ya Kagera Sugar na Simba iliyofanyika Aprili 2, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.  Pia Kamati ilibaini kuwa Banda alifanya kitendo cha aina hiyo kwenye mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Awali, Klabu ya Kagera Sugar iliwasilisha malalamiko dhidi ya kitendo cha beki wa Simba, Abdi Banda kumpiga ngumi kiungo wao George Kavilla wakati akiwa hana mpira, na Mwamuzi wa mechi hiyo kutochukua hatua yoyote. "Kwa vile kosa hilo ni la kinidhamu, Kamati imemsimamisha Abdi Banda kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) wakati akisubiri suala lake kusikilizwa na k

SOMA MAGAZETI YA LEO TAREHE 8/4/2017 INGIA HAPA USOME

leo ni April 8  2017   kila siku alfajiri nimekusogezea habari kubwa kwenye Magazeti kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia ya  Udaku ,  Hardnews  na  Michezo  ili ujue kinachoendelea 

MOURINHO AMEFANYA MAAMUZI KUHUSU JANUZAJ

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa amefanya uamuzi kuhusu winga wa klabu ya Manchester United Adnan Januzaj lakini akakataa kusema uamuzi aliochukua. Januzaj ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 22 amehudumu msimu wote kwa mkopo katika timu ya ligi ya Uingereza Sunderland ambapo itacheza na United siku ya Jumapili. Ana kandarasi ya hadi 2018 katika klabu ya Manchester United. ''Nimeamua lakini sitamwambia mtu yeyote'', alisema Mourinho siku ya Ijumaa wakati alipoulizwa kuhusu hatma ya Januzaj. Amefunga mabao 5 katika mechi 63 za United. Januzaj alihudumia miezi minne katika mkopo katika klabu ya Bundesliga Borussia Dortmund msimu uliopita, lakini alicheza mechi 12 pekee kabla ya kurudi katika timu yake ya Manchester United.

DIAMOND AMJIBU GWAJIMA SOMA HAPA ALICHOANDIKA

Hazijafika saa 72 toka mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz aachie wimbo mpya ambao unagusia yanayoendelea sasa hivi Tanzania ambapo baada ya Askofu Gwajima kuusikia, alitumia time yake kupost kwenye Instagram yake haya maneno hapa chini. Baada ya Diamond Platnumz kuona post hiyo ya Askofu Gwajima ameyaandika yafuatayo >>> “ Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba ….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu  @Bishopgwajima “ “Nilisema: “ mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza na wote kufurahi kwa pamoja ” “Lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu z