Ticker

6/recent/ticker-posts

MOURINHO AWAPONDA WASHAMBULIAJI WAKE

Meneja wa Man United Jose Mourinho

Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amewalaumu washambuliaji wa yimu yake ya Manchester United katika mechi dhidi ya Anderlecht baada ya timu hiyo kusawazisha katika dakika za mwisho za mechi ya robo fainali ya kombe la Yuropa.
United iliongoza 1-0 nchini Ubelgiji hadi dakika 86 wakati waandalizi wa mechi hiyo waliposawazisha ikiwa ni shambulio lao la kwanza.
''Iwapo ningekuwa mlinzi wa man united ningekasirishwa sana na washambuliaji,alisema Mourinho''.
''Mabeki walifanya kazi ya kutosha lakini washambuliaji wakashindwa kuamua matokeo ya mechi hiyo'',alisema Mourinho

Post a Comment

0 Comments