Wakati huu ambao kila mtu anapambana nahali yake, ujasiriamali umekua kimbilio la vijana wengi, kama tunavyojua hakuna mtu anaeanzisha kitu kwa lengo la kufeli , japo sio wote hufanikiwa. Leo nawaletea sifa 4 za wajasiriamali waliofanikiwa na pengine ukiziiga, unaweza kuongeza nafasi ya kufanikiwa katika mishe zako. 1. PENDELEA KUAMKA MAPEMA Huwezi fanikisha malengo yako kama wewe ni mtumwa wa usingizi. siku zote pendelea kuamka mapema ili uweze kukamilisha kazi zilizobaki au ngumu ambazo unatakiwa uzikamilishe kwa siku husika maana akili yako inakuwa bado ina nguvu ya kufanya mambo mengi na kwa ufanisi wakati wa asubuhi. mabilionea wengi duniani ikiwemo Mo Dewji, Bakhlesa, Dangote n.k. wana tabia ya kuamka mapema 2. PANGA SIKU YAKO MAPEMA Ni vizuri kupangilia siku yako mapema ili kujua uamkapo utaanza na nini. Hii husaidia kazi zako kufanyika kwa mpangilio na kuokoa muda ambao utaruhusu akili yako kufanya kazi na kuvumbua vitu vya nyongeza. Pia itapelekea kuboresha bi