Je, waweza kulipia kila herufi kupiga soga mtandaoni?

mtandaoHaki miliki ya pichaEXPENSIVE CHAT
Je, kwa wewe mtumiaji wa simu ya mkononi na mitandao ya kijamii, umeshawahi kuwaza idadi ya herufi unazoandika katika mawasiliano kwa jamaa na marafiki zako au kutoa maoni au mawazo yako mitandaoni kuwa ipo siku huenda usimudu gharama yake?.
Marc Kohlbrugge mjasiliamali wa mitandaoni ameanzisha ukurasa wa kupigia soga maarufu kama 'chat room', ambapo gharama yake kwa kuandika herufi moja ni kiasi cha dola 0.01 sawa na shilingi 23 za kitanzania kwa herufi moja.
gharama
Marc amesema kuwa alianzisha ukurasa huo kama majaribio yake mtandaoni, lakini amesema mwitikio wake umekuwa mkubwa kwani hadi sasa ana watu 100 ambapo hadi sasa wamekwisha mlipa kiasi cha dola 335 sawa na shilingi 785,000 za kitanzania, kwa herufi 33,0500 ambazo wamekwisha zilipia.
Suala la kupiga soga lilivyo zoeleka kwa sasa katika nchini za Afrika, Afrika Mashariki ikiwemo, sidhani kama kuna mtu anayeweza kumudu gharama,maana wapo watu ambao,tangu asubuhi hadi jioni kwa uchache anaweza kuandika herufi 1000 sawa shilingi 23,000 ambazo ukizidisha kwa mwezi ni 690,000 hapo itakuwa ni kuchagua kunyoa ama kusuka.
Kwa sasa wengi waliojitosa katika uga huo wa kulipia wa kupiga soga wanatokea Urusi, japo kuwa mwanzilishi mfumo wa kupiga soga kwa kulipia kila herufi anasema anaendelea kupokea maombi mengi tu na anataraji atapata watu kutoka nje ya Urusi pia.
chat
Marc Kohbrugge anasema aliwaza pia kuwa mtandao wake huo utatumiwa na watu maarufu na wenye pesa kwaajili ya kufanya changizo kusaidia watu wenye mahitaji kutokana na herufi zinazolipiwa na wapiga soga.
Duniani Bwana jambo unalodhani kwako ni gumu na lenye gharama wapo wanaoona linawezekana,kulipia herufi moja moja huenda ni jambo linaloweza kuwafanya baadhi ya watu kurejesha mfumo wa zamani wa Soga za ana kwa ana na ambazo hazina gharama.

Post a Comment

Previous Post Next Post