Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2017

MAUAJI DAR: Maiti tatu zadaiwa kuokotwa ufukweni Coco Beach

  ​ Maiti za wanaume watatu zimekutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo kati ya hizo moja imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba. Wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo wamesema juzi wakiwa kwenye biashara zao asubuhi ghafla waliona maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikifungwa na kamba. Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi na kuichukua kwenye gari lao. Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alitoa taarifa polisi baadaye zilichukuliwa. "Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona jana ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake," amesema Ally. Mfanyabiashara mwingine Issa Isaya amesema cha kushangaza maiti zinazo

Mwigulu Nchemba: Aliyemtisha Nape kwa bastola sio Polisi. Uchunguzi wa Lissu kushambuliwa unaendelea, tutatoa taarifa

Waziri wa mambo ya ndani atafanya mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 na watangazaji wanadhamiria kumuuliza juu ya matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana. Wale mlio majumban mkiangalia mtupe updates sisi tusio karibu na luninga. Asubuhi njema. Tutegemee siasa chafu hapo =============================================== KUHUSU MAUAJI YA KIBITI => Natoa pole kwa familia zote zilizopoteza watu wake. => Jukumu la kwanza kubwa la serikali ni usalama wa kila raia na ikitokea kushambuliwa au kuuliwa kwa mtanzania yoyote hilo ni pigo kwetu. => Kama wizara haki ya kwanza tunayoilinda ni usalama wa kila mtanzania. => Hatutaruhusu uhalifu utawale eneo lolote lile la nchi yetu na swala la kukabiliana na uhalifu halina ukomo. => Hata pale panapokuwa salama bado tutaendelea kulinda na sio kubweteka. => Hatukuchelewa kwenda kibiti mauaji yalipoanza ila ni kutokana na muundo wetu wa vyombo vya usalama. Tulikuwepo kibiti na ni suala la muda tuu. => Swala la mapambano na

MAHAKAMANI: VIGOGO WALIOKWEPA KODI NA KUSABABISHA HASARA YA BILIONI 29

Upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia hasara ya Tsh Bilioni 29 Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ inayowakabili watu watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka hiyo, Reuben Mwakasa, bado haujakamilika. Mbali na Mwakasa, mkazi wa Msagara, Moshi, Kilimanjaro, washitakiwa wengine ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, mkazi wa Makongo Juu. Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika ambapo, baada ya kueleza hayo Hakimu Mwijage ameahirisha kesi hiyo hadi October 11, 2017. Washtakiwa hao wanadaiwa walitenda kosa hilo, kati ya November 22, 2013 na August 21, 2017, katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Temeke na Ilala. Inadaiwa washitakiwa hao kwa pamoja vitendo vyao waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho kwa kukwepa kulipa kodi.

SERIKALI YATAKA MKANDARASI MPYA WAKUTOA TIKETI PINDI UWANJA WA TAIFA UTAKAPOFUNGULIWA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba pindi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam utakapokamilia kufanyiwa ukarabati atahakikisha anapatikana Mkandarasi Mpya mwenye vigezo na ambaye ataleta mabadiliko hususani katika utoaji tiketi kulingana na namba za viti vilivyopo ndani ya Uwanja huo. Kauli hiyo ameitoa jana Mkoani Mtwara wakati alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Nangwanda ili kujionea miundombinu ya uwanja huo ikiwemo baadhi ya changamoto zinazoikabili kiwanja hicho. Dkt. Mwakyembe ameeleza kwamba, kumekuwa na changamoto ya kutofahamika idadi kamili ya watu wanaoingia ndani ya uwanja hali inayopelekea watu kukaa ovyo katika sehemu zisizo rasmi na wengine kulundikana nje ya uwanja wakati pesa za viingilio wamelipia ambapo ameweka wazi kuwa hali hiyo inasababishwa na urataibu mbovu wa utoaji tiketi. Akiongea na Uongozi wa Uwanja huo wa Nangwanda Mkoani hapo alisema kwamba, kwakuwa sasa Uwanja wa Taifa uko katika ukarab

TANZANIA INA DENI LA SHILINGI BILIONI 35 ZA MATIBABU NJE YA NCHI

Serikali imesema deni linalotokana na gharama za matibabu nje ya nchi limefikia Sh35 bilioni na kuitaka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha inatoa rufaa kwa kuzingatia taratibu. Akizungumza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutibu magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa ndani ya nchi kwa kuwa imeshasomesha wataalamu wa kutosha na kwamba vifaa pia vipo. Ummy alisema nchi imekuwa ikitumia Sh5 bilioni kila mwaka kwa ajili ya matibabu nje na kwamba magonjwa ya saratani na upandikizaji wa vifaa vya usikivu yanaigharimu zaidi Serikali. “Hivi sasa deni la matibabu nje ya nchi linafika Sh35 bilioni na hilo ni deni la miaka minne iliyopita,” alisema Ummy. “Kwa sasa tumepunguza kwa kuwa wale ambao tulikuwa tunawapeleka nje kwa ajili ya kwenda kuwekewa vifaa vya usikivu ambao tulikuwa tunatumia zaidi ya Sh2 bilioni kwa mwaka, sasa tunafanyia ndani ya nchi hatutumiia fedha nyingi,” alisema Ummy. Kuhusu matibabu nje ya nchi, Ummy

MICHEZO; KIUNGO HUYU WA SIMBA SC AJIPANGA KUFUNGA MAGOLI MENGI ILI ACHUKUE KIATU

Kiungo wa pembeni wa Mnyama Simba, Shiza Ramadhani Kichuya, ameeleza kuwa, kuna uwezekano wa yeye kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu licha ya kuanza msimu kwa kusuasua tofauti na waliopo juu yake kwa mabao. Kichuya ambaye alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar, msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi hicho alifunga mabao 12 nyuma ya vinara Simon Msuva na Abdulrahman Mussa waliofunga mabao 14. Kwa sasa Emmanuel Okwi wa Simba ndiye anayeongoza kwenye orodha ya wafungaji katika ligi hiyo akiwa na mabao sita aliyoyafunga baada ya kucheza mechi tatu kati ya nne ambazo timu yake imeshacheza, akiwa na asilimia kubwa ya kuwa mfungaji bora msimu huu, huku Kichuya naye akiwa amepania kumpiku. Kwa msimu huu, Kichuya kwenye mechi nne alizocheza mpaka sasa, amefunga mabao mawili tofauti na msimu uliopita ambapo kwenye mechi nne za mwanzo alifunga bao moja. “Naamini bado nina uwezo wa kufunga kutokana na ligi bado ni mbichi sana na pia hao waliotangulia kufunga na

TAZAMA HABARI MAGAZETINI LEO JUMATANO 27.9.2O17

kila siku ni wajibu wangu kukusogezea yale yote yaliyoandikwa kwenye magazeti mbalimbali karibu kuyatazama magazeti yote siasa, michezo,burudani, udaku namengineyo                                

KOREA KASKAZINI ILIVYOMFANYIA MATESO RAIA WA MAREKANI

Wazazi wa Otto Warmbier wameelezea hali ya kutisha iliomkabili mtoto wao alipowasili nyumbani kutoka Korea kaskazini. Fred na Cindy Warmbier wameliambia shirika la habari la Fox and Friends kuwa Watu wa Korea kaskazini ni “magaidi waliomtesa mtawalia” mtoto wao. Mwanafunzi huyo wa Marekani alifungwa Pyongyang mnamo 2016 kwa kuiba kibandiko cha hoteli. Aliachiwa kwa misingi ya matibabu mnamo Juni mwaka huu lakini aliwasili nyumbani akiwa mahututi na alifariki siku chache baadaye. Korea kaskazini imekana daima kumtesa Warmbier. Inasema aliugua bakteria ya neva mwilini lakini madakatari wa Marekani hawakugundua bakteria yoyote. Hii haikuwa ajali’ Katika mahojiano yao ya kwanza tangu kufa kwake, wameliambia shirika la habari la Fox news kwamba “wanahisi umewadia muda kusema ukweli kuhusu hali iliyomkabili Otto”. Madakatari Marekani walisema alikuwa katika hali ambayo mwili wake ulikuwa hauitikii, lakini familia ya Warmbiers wanasema kuita hali hii coma “sio haki”. Bi War