Skip to main content

Posts

RC Makonda akabidhiwa ripoti ya wezi wa vifaa vya magari Dar, 73 mbaroni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa ripoti ya wezi wa magari pamoja na vifaa vya magari na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Lucas Mondya ikiwa ni miezi kadhaa toka mkuu huyo aliagize jeshi hilo baada ya matukio ya namna hiyo kushamiri ndani ya mkoa huo. RC Makonda akionyeshwa na DCP, Mkondya baadhi ya vifaa vya magari vilivyokamatwa. Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi hii wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lucas Mondya alisema katika opesheni hiyo kali jumla ya wahumiwa 73 wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, power windows, radio, injector pump, starter na seat cover. “Tarehe 19 mwezi wa saba mweshimiwa RC Makonda ulitoa maagizo kwa jeshi la polisi kwamba unatupatia siku saba kuhakikisha tunasambaratisha mtandao wa wezi wa vifaa vya magari pamoja na magari baada na sisi tumelitekeleza hilo tayari kuna watu 73

Neymar ataka kuzichapa uwanjani atupa jezi ya barcelona mazoezini

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar Dos Santos leo ametawala upya vichwa vya habari  baada ya kuvua jezi ya mazoezi ya Barcelona na kuondoka uwanjani. Neymar alikuwa mazoezini na katika hali ya kawaida kulitokea kutokuelewana kati yake na mchezaji mpya wa klabu hiyo Nelson Semedo ndipo Neymar alipokasirika. Neymar alionekana kutaka kumkabili Semedo lakini wakati anamfuata huku akionekana mwenye hasira ndipo Sergio Bosquet na Javier Mascherano walimzuia. Baada ya Neymar kuzuiwa kuendeleza ugomvi alivua jezi maalumu ya mazoezi (bibs) akaitupa pembeni kisha akaupiga mpira kwa hasira na kuondoka zake. Neymar amefanya tukio hilo katika kipindi hiki ambacho anahusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu ya PSG na huku ikitajwa kwamba hana furaha na Barcelona. Tukio hili limezidi kuongeza tetesi kwamba Neymar anaweza kuondoka Barca lakini Barca kwa upande wao pia wamechoshwa  na tabia za Neymar haswa starehe zake.

Real madrid kuvunja record ya dunia

Baada ya vilabu vingi kuhusishwa kumsajili mchezaji chipukizi wa Monaco, Kylian Mbappe, hatimaye klabu ya Real Madrid imetangaza kufikia makubaliano na Monaco kumsajili mchezaji huo. Madrid imetangaza kuwa itamsajili Mbappe kwa pauni milioni 161 ambazo kwa pesa ya kibongo inafikia bilioni 360, uhamisho ambao utavunja rekodi ya dunia ya usajili iliyokuwa ikishikwa na Paul Pogba aliyesajiliwa na Man United kutoka Juventus kwa pauni milioni 89. Mbappe mwenye umri wa miaka 18 tayari amekuwa na kiwango kikubwa cha soka ambacho kinazivutia klabu nyingi barani Ulaya iwapo uhamisho huo utafanyika kama umevyotangazwa basi atasaini mkataba wa miaka sita. Uamuzi wa Real Madrid kumsajili Mbappe umekuja ikiwa ni siku kadhaa kupita baada ya kumuuza mshambuliaji wake Alvaro Morata kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, Chelsea na kumtoa kwa mkopo kiungo James Rodriguez kwa mkopo kwenda Bayern Munich ya Ujerumani. credit http://dewjiblog.co.tz/

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULY 25,2017

Fifa yampa kifungo Bailly

Shirikisho la soka barani Ulaya ‘UEFA’limemfungia beki wa Manchester United Eric Bailly   kucheza michezo mitatu kutokana na kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Europa League dhidi ya Celta Vigo. Bailly alitolewa nje katika mchezo wa pili wa Europa League katika sale ya 1-1 dhidi ya Celta Vigo uliopigwa katika dimba la Old Trafford na alikosa mchezo wa fainali dhidi ya Ajax. Mchezaji huyo alonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na ugomvi na mshambuliaji wa Celta Vigo John Guidetti katika mchezo Kamati ya nidhamu ya UEFA imemuongezea adhabu EricBailly kwa kumfungia kukosa michezo mitatu hii ikimaanisha kwamba ataukosa mchezo wa fainali ya Super Cup dhidi ya Real Madrid. Eric Bailly katika ugonvi na mchezaji wa Celta Vigo Man United imefuzu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na kwa adhabu aliyoipata  beki huyo raia wa Ivory Coast atakosa pia mchezo wa ufunguzi wa michuno hiyo.

Simulizi ya mapenzi

Nilikua mwajiriwa katika kampuni moja maarufu jijini dare s salaam , katika kuajiriwa kwangu huko nikawa msaidizi maalumu wa bosi wa kampuni ile , basi siku moja moja nilikuwa naenda kujirusha na bosi wangu .   Ukizingatia kwamba sikuwa na mume wala mchumba na kwa kweli huyu bosi ndio alikuwa mtu wa kwanza kufanya nae tendo la ndoa , hivyo nilifurahia mhemko wake na jinsi alivyokuwa ananipenda na kunijali kila kitu nilipata na zaidi . Alifanya yote haya bila kunificha kwamba ana mke na watoto nyumbani kwake kwahiyo wakati mwingine chochote kinaweza kutokea nijiandae kwa shuguli hiyo pevu kama mke wake akishitukia dili hilo . Tulikuwa na uhusiano na huyu bosi kwa miezi 4 hivi mpaka siku moja katika tembea tembea mitaani nikakutana na kijana mmoja mtanashati akanieleza kwamba ananipenda na kunizimia sana yaani ameshanifia Huyu kijana alihangaika kwa mwezi mzima mpaka siku nikaja kumkubalia akawa ndio mpenzii wangu halali sasa , nilimwamini sana nay eye aliniamini sana , miezi 3 t

RAIS Magufuli Afunguka...Siogopi Kufungwa.......

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ‘JPM’ amesema yeye kama kiongozi mkuu wa nchi haogopi vitisho vya kufungwa ama kushtakiwa vinavyotajwa na baadhi ya wanasiasa baada ya kuwashughulikia wawekezaji wanaokiuka mikataba na kuhujumu uchumi wa nchi na badala yake ataendelea kuwatetea Watanzania wanyonge ili wapate haki yao. JPM ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini humo. “Hii nchi imejaa mafisadi, wamo wa CCM, Chadema, CUF, ACT, wazungu na wengine hawana chama. “Siogopi kufungwa, kama mliniteua niwatetee, nitawatetea kwa nguvu zangu zote juu ya majizi, tumeibiwa vya kutosha, madini yetu yanachimbwa yanapelekwa nje na hatupati kitu. “Wengine wamelipwa pesa ili kupinga tusichukue hatua dhidi ya majizi, nawaambia mimi kama rais nimejitoa kufa na kupona mpaka nihakikishe mali za Watanzania wanyonge haziibiwi na haki yao wanaipata. “Watambue kwamba sitafungwa badala yao majizi ndiyo yatafungwa. Ilikuwa lazima tubadilishe sheria zetu hatuwe