Tumeshaandika kuhusiana na huduma za Microsoft Office, hasa kama unataka kutumia huduma hiyo bure kwa kutumia mtandao, kama ulipitwa soma hapa. Sasa kama unataka kutumia huduma za kuandika document au kuandaa kazinge kama hizo kwa njia zingine mbadala utafanyaje?
Kaa ukijua huduma hizi mbadala zinasapoti huduma/mafaili yote ya Microsoft Office, spreadsheet, na presentation kwa aslimia 100. Kwa kifupi ni kwamba utakua kama unatumia tuu huduma za microsoft office.
Leo TeknoKona inakupa maujanja juu ya jinsi ya kutumia huduma hizo.
- LibreOffice ni ya bure kabisa, ina huduma zote zinazopatikana katika Microsoft office. Uzuri wake ni kwamba inaweza kutumiwa katika kompyuta ya aina yeyote kama vile Mac, Windows na Linux.
Soma Zaidi Kuhusu Libre Office hapa – Teknokona/libreoffice
- Apple iWork nayo ni ya bure kabisa na mkusayiko wa App nyingi ambazo zinatumika kama zile za Microsoft office. Uzuri wa hii ni kwamba yenyewe itakuwa inatumika katika Mac, iPhone na iPad. Huduma hii zamani ilikua inauzwa lakini Apple wakaamua uifanya iwe ya bure. Kingine kizuri ni kwamba hata kwa watuiaji wa Windows wanaweza tumia huduma hii kupitia mtandaoni kama wanatumia huduma ya uhifadhi mafaili ya iCloud.
- Google Docs, sasa hii ndio inaweza ikawa maarufu kuliko zingine zote, hii ni lazima utumie katika mtandao. Inachoweza kufanya ni kwamba utatumia na kuandaa mafaili yako yote ambayo yapo katika mfumo wa Microsoft office. Uzuri wake mwingine ni kwamba inahifadhi mafaili hayo yote katika mtandao wa Google Drive. Hii inamaanisha ukiwa tuu na akaunti ya google utaweza kutumia huduma hii.
Ni wazi kuwa kuana huduma nyingi ambazo zinafanana na hizi lakini kwa leo TeknoKona imekuleta zile ambazo inahisi ni nzuri zaidi na ni rahisi kuzitumia.
Post a Comment