Kila binadamu ameumbwa na kiu ya kufanikiwa katika kila kitu anachofanya. Mafanikio ndio kilele cha mlima mkubwa wa maisha ambao umejengwa kwa misingi na ngazi za mihangaiko na mitihani ambayo unapaswa kuivuka ili upumzike kwenye kilele hicho. Kwa bahati mbaya, unaposema ‘mafanikio’ wengi hufikiria kuhusu ‘utajiri’. Lakini ukweli ni kuwa kuna tofauti kati ya kuwa tajiri na kufanikiwa kiuchumi. Unaweza kuwa tajiri lakini ukawa bado hujafanikiwa. Kwa kuwa watu wanawaza utajiri kuwa ndio kigezo cha mafanikio hujikuta wakijiingiza kwenye vitendo vya ajabu kwa lengo la kujizolea mali lakini mwisho huwa wanagundua kuwa hawajafanikiwa japo jamii inahisi wamefanikiwa. Njia rahisi za Kumgeuza Rafiki kuwa ‘Mpenzi Wako’ wa Dhati Nanachoamini mimi, kufanikiwa kweli ni kutimiza malengo yako kwa ufanisi na kwa wakati, lakini mafanikio hayo yakupe amani moyoni mwako (peace of mind). Vinginevyo, utafanikiwa kwa mrundikano wa fedha huku ukitengeneza tatizo kubwa zaidi la msongo wa mawazo na u