Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

Roboti iliyopewa uraia nchini Saudi Arabia imesema kuwa ina haki ya kuwa na familia

Roboti iliyopewa uraia nchini Saudi Arabia imesema kuwa ina haki ya kuwa na familia. Roboti hiyo kwa jina la Sophia  ilitengenezwa nchini Hong Kong na kupewa uraia nchini Saudi Arabia mwezi uliopita. Roboti hiyo İimesema kuwa ingependa kuwa na familia wakati ilipohudhuria mkutano wa habari ulioandaliwa nchini UAE. Kwa mujibu wa habari roboti hiyo imesema kuwa familia ni kitu muhimu sana. Robot hiyo imesema kuwa kila mwanadamu ana haki ya kuwa na familia na watu wenye hisia sawa na yeye.Jambo hilo ni muhimu sana hata kwa roboti.Aliwaambia wanadamu wajisikie furaha kuwa na familia.

TRA kumchunguza Askofu Kakobe baada ya kumsikia akisema ana hela kuliko Serikali

 Kufuatia Kauli ya Askofu Kakobe kusema "Nina hela kuliko Serikali" sasa TRA wapanga kumchunguza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema; Watu wa Kodi (TRA) wanasema wamepokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao TRA wanaendelea na kusema; Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema Hivyo Askofu Kakobe ni tajiri sana kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania TRA wanasema wanawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe wakaanza kupitia kumbuk

Tetesi za usajili ulaya jumamosi tareh 30/12/2017

  Cristiano Ronaldo Cristiano Ronaldo ameitaka klabu ya Real Madrid kuweka bei yao ya kumuuza isiopungua £89m). Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Ureno yuko tayari kuondoka Uhispania.(Daily Record) Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, hajakaataa kuongeza kandarasi na mabingwa hao watetezi wa Uingereza licha ya madai kutoka kwa babake kwamba anataka kuhamia Real Madrid.(Independent)     Eden Hazard Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anajiandaa kumnunua winga wa Ivory Coast na Crystal Palace Zaha ili kuchukua mahala pake mshambulijai wa Chile Alexis Sanchez, 29. (Daily Star) Wachezaji kadhaa wa Arsenal walidaiwa kumshutumu mshambuliaji Alexi Sanchez kwa kuwa na tabia

una simu ya Android ?Soma utafiti huu

Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana. Uchnguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake.   Aidha simu hizo zinaweza kudukuliwa kwa kutumia matumizi ya betri yake huku utafiti ukisema kuwa simu zinazotumika karibu na kifaa cha kupeperushia masafa ya simu za kuungia mbali. Simu za kisasa ''Smartphone'' hutumia nguvu zaidi inapokuwa mbali zaidi na kifaa hicho cha kupeperushia masafa ya GSM, kwani inachangamoto tele za kungamua masafa. Matumizi ya nguvu zaidi ya shughuli zingine yanaweza kubaiishwa na ''alogarithm'' muundo msingi wa simu yenyewe. Watafiti hao sasa wameunda mfumo ambao unakusanya habari kuhusu matumizi ya betri ya simu. ‘’Mfumo huo hairuhusu kutumia GPS wala huduma zozote kwa mfano mtandao wa Wi-fi ‘’ Jopo hilo linajumuishwa Yan Michalevsky, Dan Boneh na Aaron Schulman kutoka idara ya sayansi ya tarakilishi ka