Katika kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linamalizika hapa nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa Serikali itajenga bwawa la kuzalisha umeme katika mbuga za wanyama Selous.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea katika vya sabasaba jijini Dar es salaam.
Amesema bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2100 ambapo zikijumuishwa na Kinyerezi 1 na 2 zitakuwa 4000 hivyo kusaidia kupunguza tatizo la umeme.
“Hatutasikiliza suala la kasoro za kimazingira za uchimbaji wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme kwa sababu Seloue iko Tanzania na umeme ni wa Watanzania,”amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo, Rais Magufuli amewaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kusaidia katika masuala ya kujenga uchumi wa nchi kwani Tanzania ina maliasili nyingi na ni sehemu yenye amani pia inawakaribisha wawekezaji wote kuja kuwekeza Tanzania.
Post a Comment