Njia rahisi ya kutumia akaunti mbili za facebook kwenye simu moja




Zaidi ya watu bilioni wantumia facebook, Facebook ni mtandao wa kijamii ambao unakuwa kwa kasi zaidi. Kwenye vifaa vya Androif tunaweza
kutumia Facebook moja katika Facebook official App na ili tuweze kutumia akaunti mbili tunatakiwa ku-logout katika akaunti kisha ndo u-log in katika akaunti nyingine.
Lakini pia kwa kutumia njia hii inachukua mda mrefu hivyo Bongo Techno tumeamua kushare Njia rahisi ya kutumia akaunti mbili za facebook katika simu moja.

Jinsi ya kutumia Facebook mbili katika simu moja

Ili uweze kutumia Facebook Mbili unatakiwa utumie App ambayo itakufanya utumie akaunti mbili katika simu yako kwa kuchagua tu akaunti unayotaka

1. Kwanza kabisa unatakiwa U-install App ya FreindCaster
2. Baada ya ku-install, Fungua App hiyo kisha utaona kama hivi :
3. Login katika akaunti yako
4. Baada ya kuingia katika akaunti yako, Sasa Bofya kwenye SETTING
5 . Kisha Chagua "ACCOUNTS"
6. Baada ya hapo utaona akaunti yako ya mwanzo, kisha utabofya kwenye "ADD ANOTHER ACCOUNT"
7. Kisha uta-log in katika akaunti yako nyingine
Baada ya kufanya hayo yote hapo juu utaweza kutumia akaunti mbili au zaidi za Facebook kwa urahisi zaidi. Hivyo ili uweze kutumia akaunti nyingine unatakiwa kubofya kwenye SETTING>>ACCOUNTS then utachagua akaunti unayoitaka........

Post a Comment

Previous Post Next Post