MWAMUZI AONDOLEWA KUCHEZESHA LIGI KUU VPL

Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi za Tanzania (Kamati ya Saa 72), imemwondoa Mwamuzi wa kati, Ahmada Simba katika orodha ya waamuzi watakaochezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.
Hatua hii imefikiwa baada ya utetezi wa Mwamuzi Simba kudai kwamba hakuona tukio la Mchezaji wa Young African, Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa na kumwonya mchezaji kwa kadi njano.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo ambao Young Africans walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka huu.
Katika hiyo ya njano ilikuwa ni ya kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta kadi hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.
Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.
Kufutwa kwa kadi ya njano ya kwanza, kunapelekea kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo ulisababisha kadi nyekundu hivyo mchezaji angempaswa kukosa mchezo mmoja. Hata hivyo, kadi ya pili ya njano inahesabiwa.
Kadhalika uamuzi mwingine ulikuwa ni kuipiga faini Young Africans iliyocheza na Simba Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Wanajwani hao kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi. Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini tano).

Post a Comment

Previous Post Next Post