Mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika jana Jumapili mjini hapa, yameacha simanzi baada ya mwanariadha Mkenya, Charles Maroa (36), kufariki dunia baada ya kuanguka ghafla alipomaliza mbio hizo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polis Mkoa wa Kilimanjaro, Willbroad Mutafungwa, mwanariadha huyo alipoanguka, alipewa msaada wa kuwahishwa Hospitali ya KCMC lakini alipofikishwa hospitalini hapo madaktari walibaini kuwa alishafariki. Mkenya huyo alikuwa akishiriki mbio za Kilomita 21 katika mbio hizo zilizoshirikisha wakimbiaji mbalimbali wa kimataifa na kushuhudia Mtanzania, Emmanuel Giniki, akifanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza. Chanzo: Mwanaspoti
mwanariadha mkenya afariki dunia
dody
0
Post a Comment