Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2017

tutanchukulia hatua aliyempa makonda kwanja

Lukuvi kumchukulia hatua aliyempa kiwanja Makonda. Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara aliyemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa kuwa eneo hilo sio lake ni mali ya serikali."Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu," alisema Lukuvi. Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara aliyemkabidhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Pau l Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa sababu eneo hilo si lake ni mali ya Serikali. “Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu,”amesema Lukuvi leo (Jumatatu) katika mkutano na waandishi wa habari. Lukuvi amesema anataka watu wote wanaomiliki maeneo mijini kujisalimisha kwa maofisa ardhi wa wilaya wa ajili ya uhakiki. Chanzo: Mwananchi

mwanariadha mkenya afariki dunia

Mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika jana Jumapili mjini hapa, yameacha simanzi baada ya mwanariadha Mkenya, Charles Maroa (36), kufariki dunia baada ya kuanguka ghafla alipomaliza mbio hizo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polis Mkoa wa Kilimanjaro, Willbroad Mutafungwa, mwanariadha huyo alipoanguka, alipewa msaada wa kuwahishwa Hospitali ya KCMC lakini alipofikishwa hospitalini hapo madaktari walibaini kuwa alishafariki. Mkenya huyo alikuwa akishiriki mbio za Kilomita 21 katika mbio hizo zilizoshirikisha wakimbiaji mbalimbali wa kimataifa na kushuhudia Mtanzania, Emmanuel Giniki, akifanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza. Chanzo: Mwanaspoti