Skip to main content

Posts

MTU WA NGUVU MASTER PASS ANAKUALIKA KUITAZAMA VIDEO YAKE MPYA

Ingia hapa kuitazama bonge moja la kichupa>>>>>>> https://youtu.be/WhvQh0-o84A

GWAJIMA AWAKA AMJIA JUU DIAMOND

Ni masaa machache tu toka Diamond aachie wimbo wake mpya 'Acha nikae Kimya' ambapo amewataja baadhi ya watu maarufu ikiwemo mchungaji Gwajima. Baada ya Mchingaji huyo kusikiliza huo wimbo ameweka picha kwenye instagram yake na kusema maneno haya "Aliyeniweka kwenye wimbo kwa leongo la kupotosha haki ili kupotosa vyeti feki jiandae Almasi itageuka Maji kesho!" TAZAMA WIMBO HUO HAPA CHINI KISHA USISAHAU KUSUBSCRIBE USIPITWE NA KITU

SPIKA WA BUNGE ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMKAMATA HALIMA MDEE

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017. Pia Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi huo  wa EALA.  Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo  na anatakiwa kufika leo.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 7,2017

Nimekusogezea vichwa mbalimbali vya habari katika magazeti mbalimbali tanzania katika michezo, burudani, siasa bila kusahau katika udakui Magazetini leo Ijumaa Aprili 7,2017

UEFA Europa League WAMZUNGUMZIA MBWANA SAMATA WAMEANDIKA HIVI

Tukiwa tunaelekea kutazama michezo ya kwanza ya robo fainali ya  UEFA Europa League  alhamisi ya April 13 2017, jina la mtanzania  Mbwana Samatta  limezidi kuchukua headlines katika michuano hiyo,  Samatta  na timu yake ya  KRC Genk  watacheza mchezo wao wa kwanza wa robo fainali dhidi ya  Celta Vigo  ya  Hispania . Leo kupitia ukurasa rasmi wa twitter account ya  UEFA Europa League  wamelitaja jina la mtanzania  Mbwana Samatta  kwa kumpost katika twitter account yao na kuuliza swali  je huyu ni wa kumuangalia? hiyo ni baada ya  Samatta  kuonesha uwezo mkubwa akiwa na  Genk  katika mechi 5 zilizopita. Samatta  katika mechi tano zilizopita za  KRC Genk  za mashindano tofauti amefanikiwa kufunga jumla ya goli 6 hivyo  Samatta  kwa takwimu hizo anatajwa kama mchezaji wa kuangaliwa,  Genk  watacheza mchezo wao wa kwanza wa  Europa League  ugenini dhidi ya  Celta Vigo  nchini  Hispania  katika uwanja wa  Balaidos  saa 22:05 kwa saa za Afrika Mashariki.

TETESI; ZLATAN KUTIMKIA MAREKANI

Staa wa kimataifa wa  Sweden  ambaye anaichezea  Man United  ya  England   Zlatan Ibrahimovic  ni wiki kadhaa sasa amekuwa akihusishwa kuelekea kujiunga na  LA Galaxy  ya Ligi Kuu Marekani,  Zlatan   hadi sasa ameichezea  Man United  game 41 na kuifungia goli 26 akitoa assist 9 katika mashindano yote. Uvumi wa staa huyo kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kwenda kujiunga na  LA Galaxy  ya  Marekani  unazidi kuwa mkubwa kutokana na staa huyo kutosema chochote kuhusiana na msimamo wake licha ya kuwa kocha wa  Man United  Jose Mourinho  mwezi uliyopita alisema wanasubiri maamuzi ya  Zlatan . Kituo cha TV cha Marekani kinachojihusisha na michezo  FoxSports  kimeandika stori kupitia ukurasa wake wa instagram  foxdeportes Verified  imethibitika kuwa  Zlatan  anakuja kutokea Ulaya huku picha yake inayoaminika ya kutengeneza ikionekana kavaa jezi za  LA Galaxy . Kama taarifa za  Zlatan Ibrahimovic  zitakuwa  za kweli kuwa ataondoka  Man United  mwisho wa msimu akiwa kamaliza mkataba wake,

YALIYOJILI KATIKA MAGAZETI LEO TAREHE 6/4.2017 KARIBU AMKA NA HABARI MAGAZETINI

Good Morning, leo ni April 6  2017  nimekusogezea vichwa mbalimbali ya habari katika magazeti karibu uweze kuhabarika, amka na habari mambo mengi yameandikwa katika magazeti mbalimbali ya kisiasa, michezo pamoja na burudani bila kusahau katika magazeti ya udaku